DOKEZO Vibaka wanaotumia boda wanakata watu mapanga Mchana kweupe maeneo ya Kimara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna siku watafanya hivyo tena kisha bodaboda itafeli hakutakuwa na wala kumlaumu.
 
Wakati natokea KIBAHA PWANI nafika GEITA nilizani jambazi akishika AK 47 hawezi kutulizwa lakini siku Moja majbazi Saba wakiwa wenye bunduki 4wengine 3wanamapanga walivyovamia miji kama 5 hivi mwano ulilia kijiji chote mpaka jirani police wakajificha lakini ile hofu ya mwano majambaza wawili tu ndio walipona mmoja alichomwa na Mkuki wakuulia Fisi akiwa na silaha yake wengine wakajificha sehemu za kijinga kijinga ila Yote mikoani Kuna mtu katili
 
Matukio ya kihalifu yameanza kurejea tena kwenye baadhi ya mitaa ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa leo nitazungumzia yanayoendelea Kimara Korogwe, njia ya kuelekea KAM College kupitia mji mpya.

Ndani ya mwezi mmoja kuna watu wawili wamekatwa mapanga na vibaka wanaotumia bodaboda. Matukio haya yote yanahusisha wasichana, ambapo mmoja ilikuwa ni saa 12 jioni anatoka kazini kurudi nyumbani na tukio lingine limetokea wiki iliyopita saa 1 asubuhi mdada mwingine akiwa anaenda kazini.

Kinachofanyika kinasikitisha sana. Vijana hawa huja na boda wakiwa wamepakiana, na mara nyingi huendesha kwa kasi huku wakimpita mhusika kwenda mbele kukagua kama kuna watu, wakiona hakuna watu hurudi kwa kasi tena na kutoa panga kisha huanza kukata sehemu yoyote wayaoona inafaa.

Kwa visa hivi viwili, mmoja alikatwa taya nusu lidondoke na mwingine kakatwa mkono. Na baada ya kufanya hivi hubeba simu/mkoba wake na kutokomea nao kusikojulikana.

Kwenye tukio la wiki iliyopa, baada ya kukata mkono wa huyo dada waliendesha boda yao ya kasi sana kuelekea Maeneo ya Kimara Bucha huku wakifukuzwa na watu lakini bahati mbaya kutokana na ujenzi wa barabara unaoendeelea litokea gari katikati likaziba njia wakawa wamenusurika vinginevyo wangeuawa. Kumbuka, hii ilikuwa ni saa 1 asubuhi.

Kwasasa wananchi tumeanza kujilinda, tunaomba mamlaka za ulinzi zifike eneo hili kuimarisha ulinzi. Vinginevyo mkisikia tumeua hawa vibaka msije kutusumbua.

========================

MKUU WA WILAYA ATOA NENO
JamiiForums imewasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Jacob Twange kuhusu hoja hiyo amesema “Hilo suala kwangu ni jipya, ndio nalisikia lakini kwa kuwa aliyezungumza ni Mwananchi na sisi Viongozi tupo kwa ajili ya Wananchi, basi saa mbili kutoka sasa, mimi pamoja na Viongozi wa Jeshi la Polisi Ubungo tutaelekea hapo.”

Ameongeza “Tutaenda kuonana na Serikali za Mtaa kisha tutazungumza na Wananchi tusikie maoni yao kujua kinachoendelea, hiyo itatusaidia kujua tunachukua hatua zipi za kuchukua.”
Ni jambo la kumshukuru mheshimiwa rais k
 
Dah! Kwa kweli hao mkiwadaka muwafanyie chochote tu maana hawana ubinadamu kabisa
 
Hebu angalia matukio kama hayo harafu polisi wanapoamua kufanya kazi humu humu kelele zinaanza wasiojulikana wanawateka watu,, chomboni cha usalama hakifanyi kazi ngumu kwakutambulika kwa haraka ndani ya jamii ili kukamilisha majukumu, ukiona mtu mpaka anakamatwa mahali popote pale ujue hatua za kiuchunguzi zimefanyika kwa kina! Mim nikupongeze Sana kwa taarifa hii imetoa funzo, yule boda aliyekamatwa kibaha watu waliongea mengi Sana,, Malipo ni hapa hapa
Shida sio kukamata watu. Shida kukamata halafu hawaonekani tena.

Imagine anachukuliwa kaka yako hapo halafu humuoni tena.
 
Mkiwakamata wakatumike kama skeleton za mafunzo mashuleni baada ya kuwaengua nyama zao.
 
Binafsi juzi kati hapa Kuna vibaka watatu wamewakaba wadogo zangu wawili(wa kike) wakawapiga,wakawapora pesa za mauzo yote ya dukani na simu ya mkononi( smart phone). ktk hao vibaka mmoja walimtambua/ tumemtambua maana muda mwingi alikuwa akionekana pale mtaani kwetu.

Sasa baada ya hilo tukio kibaka huyo ametoweka mtaani na haonekani tena, namtafuta !! Nikimnasa!! Na nitamnasa tu!! Atawataja wenzie wote aliokuwa nao! Sina haraka nae Wacha akimbie kimbie tu
Hawajawala mzigo
 
Huku Kibamba kuanzia Luguruni Kibamba Hospital mpaka Chama wanatamba tu.. Imefikia wakati Watu tunatembea wawili wawili . Ukiwa peke yako lazima ubebe silaha.. Vinginevyo unaweza kushambuliwa muda wowote..

Lakini kwangu naona suluhisho ni kuwaua tu.. Popote atakapokamatwa kibaka wa pikipiki auwawe
 
Back
Top Bottom