Vibali vya ujenzi

Vibali vya ujenzi

Fika halmashauri, watakupa fomu ya kujaza, umpate surveyor, mchora ramani akuchoree na vingine nimesahau kuna kamlolongo.. Kisha utapewa namba ya kulipia mpunga, bei inategemeana na jengo kamani la makazi ama biashara, kama i ghorofa ama kawaida na ukubwa pia.

Mengine nimesahau.
 
Zamani ulikuwa ukipeleka maombi unasubiri baraza la madiwani likae, sijui siku hizi ikoje.
 
Utaratibu wa kupata kibali cha ujenzi ukoje ?
Mkuu kuna website hii https://tausi.tamisemi.go.tz.
Ni rahisi kufungua akounti yako/ yaani kujisajili kwa kutumia namba zako za NIDA.
Utakuta huduma mbalimbali, kama hizi.
Leseni ya Biashara​
Leseni ya Vileo​
Leseni ya Hotel​
Kibali cha Ujenzi​
Leseni ya Uvuvi​
Ushuru wa Huduma​
Ushuru wa Hoteli​
Kodi ya Majengo​

Kwenye maombi yako utatakiwa kuambatanisha hivi:
Land Rent receipts(Risiti ya Kodi ya ardhi)​
Title Deed/Offer(Hati Miliki)​
Architectural Drawing​
Fire Document​
 
Back
Top Bottom