Pole. Ila usikate Tamaa, Mi Toka Niko Mdogo, sikuaga na wazo la kuajiriwa.
Na Sijawai kuajiriwa zaidi ya Kufanya Vibiashara(ndogo ndogo) na ndo naendesha Maisha Yangu kupitia Biashara.
Pia kuhusu swala la kwenda JKT mi Binafsi nililikataa, maana niliitazama Familia Yangu, na ndugu wanaonizunguka na Marafiki, hakuna mtu Alie ktk mfumo na. Hakuna Connection.
Na nilichukua mda wangu kufanya tathimini Hawa, watu wanapataje kazi. Ukiachana na vigezo vya kazi kuna mfumo wa Connection upo Chini kwa Chini, huo Ndio unawapa watu kazi. Je huo mfumo unaupataje, na nilitazama kuhusu jinsia Yangu.
Mi Mwanaume changamoto nitakazo kutana nazo Uko JKT na Muda nitako utumia Uko, nitaufidia Vipi Endapo sitopata ajiri, Hata mkataba wao sio wa Kupata ajira inaonyesha pale Ni sehemu ya mafunzo,na wao hawatoi ajira.
Unapotaka kufanya Jambo lifanyie uchunguzi kwanza.
Ok nilitazama kwa Upande wa Mwanamke akienda JKT, kiuhalisia Ni Kama changamoto zinafanana Ila waafrika tunapenda Sana Ngono, kwa jinsia ya kike wanatumika sana.
maana Slogan ya Jeshi Ni "Yes Sir"
Akisema akatae ataishi kwa shida Sana. Ina mlazimu kukubari,
Na akipata Mimba Hilo Ni zigo lake .
Akisema ashitaki hapati msaada Hawa watu wanabebana Sana na kulindana kwa 100%.
Nilitazama kwa upande wangu, na nikaamua kuachana na mfumo wa kuomba ajiri nikachukua cheti Changu nikakitia katika begi, na kuanza kupambana kwa bishara tu, na ninachokitazama Ni Kupata Pesa ya kuendesha Maisha, ikitokea nimepata utajiri Ni sawa, shukrani kwa mwenyezi Mungu.
Kwa Sasa Nina Familia Yangu na Maisha Yana songa. Usikate Tamaa ndugu Yangu.
Angalia Jambo lingine Fanya hayo Mambo ya kuitaji kazi za Jeshi, au kuajiriwa sehemu fulani, waachieni wenye connection Zao.
Toka nimezaliwa Sijawai andika barua ya kuomba ajira.
Natoka Familia ya Kawaida Sana.
Familia Yetu tuko watu wacheche Sana.