GreatThinkers,
Ni kweli kuna mabasi manne yalikamatwa Jomu-Tinde, watu mamehojiwa na baadaye wameruhusiwa.
Ifahamike pia kuwa Tinde ni kata ili iliyo Jimbo la Solwa ambalo liko Shinyanga Vijijini sehemu ambayo mwaka 2010 hapakuwa na Mgombea wa CDM bali CUF na CCM.
Hili ndilo Jimbo ambalo JeyKey oct-2010 alithubutu kutamka wakati wa kampeni akiwa kijiji cha Iselamagazi kuwa Wasukuma nyie hata mkiletewa Mchina mtamchagua tuu, hiyo ilitokana na Mwarabu mmoja darasa la nne mwenye pesa zake ambaye si chaguo lake kumshinda mtu wake na hatimaye kulichua jimbo tena.
Nataka kusema nini, Mabasi haya yametoa watu sehemu za Vijiji vya Mishepo,Ngokolo,Didia (luhumbo), Samuye, Nsalala, Mendo nk katika Jimbo hilo la Solwa.
Jamaa wameruhusiwa na nadhani saivi wamekaribia Nzega, kuna kila dalili kuwa hao ni watu wa Si Si Em, tatizo mawasiliano hayakuwa mazuri, Jamani kazeni uzi Igunga Si Si EM wanaleta mamluki.
Taarifa za Nzega pia mzifuatilie zinaweza kuwa za kweli kuwa kuna masanduku ya kura feki, Mwaka jana 2010 Masanduku kama hayo yalikutwa Misungwi, Jimbo amablo CDM alisimama Dada mmoja (Jane) ni shupavu ambaye nimeapa kumsapoti 2015 na yuko chini ya miaka 30.
Niwaombe ndg. kuiondoa Si Si Em inahitaji kujitoa na kuamua, bado nchi ina watu maskini na wajinga, ambayo kama wakichukia wanaghairi kupiga kura. Inashangaza sana Dar mmepumzika, Kanda ya Ziwa Si Si Em inapumulia Mashine na sasa tunakuja Igunga watu wamepata Elimu na hilo litabaki jimbo Gumu miaka yote ijayo.