Wengi wao ina maana 89% wamekutwa na kadi za cdm, hizo 11% wamesahau kadi zao home.
Swali, ukikutwa na passport ya uingereza basi wewe lazima ni muingereza, una kibarua ndugu yetu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wengi wao ina maana 89% wamekutwa na kadi za cdm, hizo 11% wamesahau kadi zao home.
Unafafana na ule wa CDM kuingiza makomandoo 33 au ule uliokiua chama cha CUF kuwa kimeingiza mapanga na visu? CCM ni mabingwa wa propaganda, isipokuwa saizi wamekutana na barrier kubwa ya uelewa wa wananchi na kiu kubwa ya kuona mabadiliko baada ya kuichoka CCM na sera zake zisizo tekelezeka.
Bibie umerudi? Habari za New York na DC?Uongo huo! nani wa kuaminika CHADEMA?
achana na huyo bwana!!Swali, ukikutwa na passport ya uingereza basi wewe lazima ni muingereza, una kibarua ndugu yetu.
Nakubaliana nawe Crashwise ila mbinu hiyo ni risk sana kwa huyo mtu na effect yake huwa si kubwa kwa vile wanaofanya hivyo ni wachache ni wale waliopata mafunzo. Kuna mbinu zenye effect kubwa kama vituo hewa yaani kati ya vituo say 427 vilivyopo 7 vinakuwa hewa, huwa tunavitambua kwa vile utashangaa ndivyo vinaongoza kwa turnout, kwenye majumuisho anakuja mtu kwenye gari from no where amebeba masanduku anasema anatokea kituo X kwa vile hamjuani mnakubali, lakini hii inatokea kama kituo hicho hakina wakala wa CDM aliye mwaminifu. Hii mbinu imetumiwa sana mikoa ya kusini Lindi Mtwara ambapo kuna baadhi ya vituo havikuwa na mawakala wa wapinzani ila kwa aibu CCM walikuwa wanatafuta watu na kuwalipa kujifanya wanawakilisha chama fulani ili kufanya watu waamini hakuna hujuma.
umeisha hara uharo tena!!panapo toka roho si mchezo lazma kuna kutapatapa,wamesha anza tayari kulalama CDM.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwa karatasi hizo pamoja na maboksi hayo ya kura yamehifadhiwa nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, taarifa ambazo zimekanushwa vikali na kiongozi huyo.
Chadema kimesema kuna njama za kuingiza kura bandia Igunga na kwamba tayari karatasi na masanduku ya kura yamefikishwa mjini Nzega kwa ajili ya kuingizwa Igunga siku ya uchaguzi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana majira ya saa tano asubuhi katika Kata ya Nkinga, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema Chadema kina taarifa za uhakika kwamba tayari karatasi hizo zimeshawasili wilyani Nzega.
Ndugu waandishi mlioko katika mkutano huu, hii ni taarifa rasmi ya chama na kwamba tuna taarifa za uhakika kwamba karatasi hizo zimehifadhiwa nyumbani kwa ofisa mmoja wa Serikali, alisema Mbowe.
Aliendelea kusema kuwa tayari karatasi hizo zimeshapigwa kura na kudumbukizwa kwenye maboksi ya kupigia kura tayari kwa kuyaingiza kwenye vituo vya kupiga kura.
Mbowe alisema kuwa tayari vijana wa Chadema wameshakwenda Nzega kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha karatasi hizo haziingii Igunga.
Mbowe aliendelea kusema kuwa mpango huo wa CCM unatekelezwa kwa msaada mkubwa wa usalama wa taifa na kuonya kuwa iwapo zinaingia Igunga basi hapatakalika.
Source: Mwananchi
BBJ mimi nakubaliana nawe asilimia 100. Nimewahi kuandika sana humu kuwa CCM kamwe haiwezi kutoka kwa sanduku la kura, zinahitajika nguvu. Wakuu CDM mkitoka Igunga itisheni maandamano Dar kuipinga CCM, Taifa sasa limeiva kwa ukombozi, hakuna haja ya kupoteza muda. Tufanye kama Libya maandamano kisha mtutu mpaka watokomee.
Taarifa kama hizi ni viashiria vitakavyopelekea uchaguzi mdogo wa Igunga usiwe wa amani. Hivi kama ni kweli mambo kama haya yapo inakuwaje Mheshimiwa Mbowe apaze tu sauti kwenye jukwaa pasipo kutoa taarifa na vithibitisho kwenye vyombo vya usalama vilivyo na jukumu la kufuatilia mambo kama haya? Hivi inaingiaje akilini CDM kutuma vijana wake Nzega kufanyakazi ambazo si majukumu yake? Kuhusisha chombo cha Usalama wa Taifa katika hili ni kukidhalilisha. Yafaa vyombo vya usalama vimpate Mheshimiwa Mbowe asaidie ili wote wanaohusika wakamatwe mara moja kabla mambo hayajakwenda ndivyo sivyo
Kama wanajua yalipo na yanavyopangwa kutumiwa kwanini wasitumie muda kupanga kuyakamata "live"? Ingekuwa ndio ushahidi mzuri kweli hasa kwenye mazingira ya digital camera na internet.. sasa yasipotokea Jumapili tutaamini kuwa yamedhibitiwa siyo? Na kama hayakuwepo? Chadema ina mawakala kwenye kila kituo?
Kulalama?panapo toka roho si mchezo lazma kuna kutapatapa,wamesha anza tayari kulalama CDM.
Kubeza taharifa c jambo zuri, bali kutafakari ni vema, ktk kutafakari kwangu napata swali moja kubwa, ilivyosasa tune radio zote, ama TV zote utakuta habari karibu zinafanana, habari hizi zilizopatikana kwenye radio ya chama tu
inawia ngumu kuamini, ingawa kwa wa Tz, yoyote anaweza kuongea chochote na lolote hata pasipo vthibitisho naye akawa ni mshindi, mbona waziri Ngeleja alisema tatizo la umeme litakwisha July, 2011, na sisi kumbe tumegeuza kalenda na tungali tumeweka mikono nyuma, Tz wanyenyekev
Taarifa kama hizi ni viashiria vitakavyopelekea uchaguzi mdogo wa Igunga usiwe wa amani. Hivi kama ni kweli mambo kama haya yapo inakuwaje Mheshimiwa Mbowe apaze tu sauti kwenye jukwaa pasipo kutoa taarifa na vithibitisho kwenye vyombo vya usalama vilivyo na jukumu la kufuatilia mambo kama haya? Hivi inaingiaje akilini CDM kutuma vijana wake Nzega kufanyakazi ambazo si majukumu yake? Kuhusisha chombo cha Usalama wa Taifa katika hili ni kukidhalilisha. Yafaa vyombo vya usalama vimpate Mheshimiwa Mbowe asaidie ili wote wanaohusika wakamatwe mara moja kabla mambo hayajakwenda ndivyo sivyo