Vibweka vya wananawake

Vibweka vya wananawake

bendee

Senior Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
111
Reaction score
146
1) Wanaweka simu zao kwenye mapochi makubwa halafu ikiita anaanza kuitafuta hajui inaitia wapi!

2) Siku zote wao wanabeba mapochi makubwa (hand bag) ambalo amejaza makororo kibao ambayo hata hana shida ya kuyatumia lakini anaamini ipo siku atayahitajia!

3) Utamuona yupo bize anaitafuta miwani yake ya jua (sun glasses ) wakati kaivalia kichwani!

4) Akiwa na haraka yakutoka utamwona anatafuta ufunguo wakufunga mlango kila kona wakati funguo zenyewe amezishika mkononi!

5) Siku zote wao wanajitizama kwenye kioo kabla kutoka kwenda kazini au kwenda nje! Na ukute ana miliki usafiri wa gari basi akiingia garini anajitizama tena kwenye kioo! Hahaha ni shidaa!

6) Utakuta kabati limejaa nguo nab ado anakuambia hajui au hana nguo ya kuvaa!

7) Akitaka kwenda msalani kama yupo kwenye semina au mkutano lazima amtafute mwenzake ampe kampani ya kwenda msalani

8) Siku zote wana wasi wasi kuhusu muonekano wa maziwa yao, mara aya hisi yamelala mara ayahisi nimakubwa!

9) Wanafikiri bia zote zina ladha sawa!

10) Anakwenda safari ya siku tatu tuu lakini kwenye begi anapaki viwalo vya siku kumi!

Hebu na wewe tupia vyengine!!!
 
🙂 from danya 🙂
Sitaki stress siku hata nikiwa sina hata mia nitaishi kwa amani hakuna wakunisumbua kuliko kuwa na mke sa nne usiku kakuomba hela unamwambia sina mnalala wote sa kumi na mbili asubuhi anakuomba tena hela hivi usiku anadhani alilala peke ake? Mimi nilikuwa kutafuta pesa? Mwisho wa siku mnaishia kugombana na kununiana hiyo mimi hapana sitaki kabisa.
 
Hiyo namba moja mpaka tulishawahi kugombani,yaani simu inaita afu anakuliza simu yangu iko wapi,simu inapotelea ndani mnaanza kuitafuta,nikaona ni uboyaaa huu
 
hahaaaaahahahaa aisehhhh na kweli kila siku kushona nguo. Sista yangu mmoja kumaliza chuo tu vitu tulivyovikuta ndani mwake tulichoka. Nguo na viatu unajaza canter sasa usihesabie urembe yaani ni begi langu la kuwekea makorokoro yangu na nafasi inabaki kubwa
 
Back
Top Bottom