Vicent Kigosi(Ray) asalimu amri baada ya kukubali kuachana na filamu yake

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,878
Reaction score
5,432
RAY ASALIMU AMRI BAADA YA KUKUBALI KUACHANA NA
FILAMU YAKE ILIYODAIWA KUWA INA UDHALILISHAJI
MKUBWA

HATIMA ya filamu ya mwigizaji, Vincent Kigosi ‘Ray’,
Sister Mary iliyokuwa imezuiwa kwa kudaiwa
kudhalilisha ukatoliki, imefahamika kuwa mwigizaji
huyo amesalimu amri ya viongozi wa kanisa hilo.

RAY.jpg

Cover la filamu hiyo ya Sister Marry.

Kanisa Katoliki nchini linaloongozwa na Muadhama
Polycarp Kadinali Pengo, liliizuia filamu hiyo kwa kile
kilichodaiwa kuwa ilikuwa ikionesha udhalilishaji kwa
namna ambavyo watawa wamevaa mavazi mafupi.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Ray amebainisha kuwa
baada ya kuambiwa achomoe vipande vingi kwenye
filamu hiyo, ameona ni bora kuachana nayo kwani hata
akitoa haitaleta maana hivyo atakujairudia upya wakati
mwingine.

“Asilimia 85 ya filamu niliigizia kanisani na ndivyo
walivyosema niviondoe, sina ujanja kwa sasa
nimeanza kushuti filamu nyingine kabisa ile labda
nije kuirudia upya hapo baadaye,”
Alisema Ray

Source : Mpekuzi
 
Hili ni tatizo kubwa sana kwa wanasanaa wetu wa tanzania kutokufanya 'utafiti' wa kile wanachokitengeneza......jamani sanaa sio 'uongo' bali ni 'ubunifu'.....kwa hiyo:
Msanii anatakiwa afanye utafiti ili kujua watu fulani...wanavaaje....wanaishije
kwa huko majuu holywood na kwingineko, bila shaka mwongozaji (dairekta) wa filamu hii angerushiwa mawe na watazamaji.
Nashauri mambo yafuatayo:
1. Wanasanaa wafanye utafiti kabla ya kutunga au kutengeneza kazi zao
2. Wajisomee vitabu vinavyoelekeza maarifa au mbinu ya kutengeneza sanaa
3. Wahudhurie masomo ya kina kuhusu sanaa....zisiwe kozi za muda mfupi kwa kuwa huwezi kuiva na kuwa nguli
4. Watumie ushauri wa wataalamu wa sanaa
5. Vyeo au majukumu katika utengenezaji wa sanaa yagawanywe kwa watu mbalimbali: Ukiwa mwongozaji, usiwe mbunifu wa mavazi, usiwe mpiga picha, usiwe mwongozaji, usiwe mpodoaji nk. Katika filamu mtu mmoja anapaswa kufanya kazi moja tu na sio mbili
6. Kukubali ukosoaji kwa ajili ya kuboresha kazi (anayekukosoa anapenda ufanikiwe...fanyia kazi kasoro alizoziibua)
7. Kuitazama filamu kupitia timu ya wataalamu na wakosoaji kabla haijawafikia watazamaji (critic panel)... Wakikukosoa wataalamu hawa unarudi uwandani kurekodi upya na kurekebishwa kasoro walizoziona kabla kazi haijawafikia watazamaji
nb: Kwa kweli mimi nilikuwa nazikubali kazi za marehemu kanumba kwa kuwa naye mwanzoni alikuwa akitengeneza kazi zenye kasoro, lakini nadhani alikuwa anakubali kukosolewa na kazi zake za mwishonimwishoni mliona wenyewe zilivyokuwa na viwango. Kwa hiyo wanasanaa tukubali kukosolewa kwa lengo la kuboresha.
Anayekukosoa hakuchukii.....tubadilike. Wasanii tusipobadilika tutaishia kuwalaumu watanzania kuwa 'sio wazalendo hawanunui kazi za nyumbani'.... Nani atafurahi kupoteza pesa yake kwa kuangalia filamu inayoudhi????? Tangu lini masista wakavaa vimini na kujifunuafunua hadharani....? Tangu lini masista wakavaa vikuku? Na viatu vya mchuchumio?? Jamani fanyeni utafiti kabla
 
ooooooopx Rl xry 4 da loss bt n wajanja hawa hawakawii kuitoa kimagendo den wakasema imevujishwa
 
Ushauri Mzuri ila watakuambia hawana Hela za kuwalipa watu wote hao kila sector.. Ila wanahela za kununulia Mbwa mavazi ya mamilioni na Kununua magari ya kifahari
 
nimemkumbuka marehem kanumba jembe la ukweli. sio huyu muuza Sura.!!
 
waache wasishaurike....zitakapowadodea ndio watakumbuka kufuata ushauri. TUTAWAFANYIA MGOMO BARIDI kwa kununua kazi kutoka sehemu zingine za Afrika....
 
Back
Top Bottom