Vichaa huona nini?

Vichaa huona nini?

Psychedelic-Purr-Purr.jpg.jpg
baadhi ya picha waonazo vichaa unapowaona wakikimbia ama kuficha nyuso

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale watu bwana kuna namna ambayo huwa nashindwaga kuwaelewa kabisaa... Wale wakorofi unaweza kuta mko watatu au wanne akampiga mmoja wenu tena kwa kumchagua kabisaa.... Au akachagua mmoja akamtusi...

Hii nimeiona mnoo zaidi ya mara tatu na vichaa tofauti yaaani lile rungu alopigwa mwenzangu kila mtu alijua mie ndo nashushiwa... Daah
wild-things-600.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naumia sana ninapomuona mtu 'mwenye matatizo ya akili'(ufahamu), wengine huita vichaa ama wendawazimu. ... Baadhi yetu tuna tabia ya kuwafukuza na wakati mwingine kuwapiga kabisa
KUMBUKA! Hawa nao ni binadamu wenye ndugu jamaa na marafiki! Wengine wana watoto... Ni jambo la kijamii linalohitaji tafakuri ya kina kwakuwa ni wachache MNO walizaliwa wakiwa vichaa.... Hujafa hujaumbika!!!!
40f7b05a246be052b1d5439f88b18dde.jpg

Turejee kwenye mada yetu!
Vichaa wako wa aina tofauti wapole waoga wakorofi wababe micharuko nknk.... Yote kwa yote hufanya vitu tofauti na kawaida yaani hutenda kinyume na mazoea
Kuna dunia ya vichaa! Kuna mawasiliano kati yao na vitu tusivyoviona sisi lakini wao wanaviona kusikia na hata kuhisi
Huwa tunasema nut zimelegea ama dish limecheza au tunawaita dakika tatu mbele
Nut zikilegea kwenye gari ama mashine lazima kutatokea sauti za ajabu
Dish likicheza lazima hutapata picha clear
Dakika tatu mbele manake hii ni foreseen.. Yani wanaona kabla ya wakati husika kufika... [emoji15] [emoji144] je hiki ndio chanzo cha uchizi wao?
Wanapokaa na kuongea pekeyao kwa mtazamo wetu... Naamini hawaongei pekeyao bali huwa na mawasiliano na viumbe visivyoonekana kwa macho yetu
Kuna viwango vya ukichaa! Mtu hawezi kuwa kichaa kwa asilimia mia moja! Na ikitokea akawa hivyo hachukui round anakufa
Lazima kuna asilimia za ufahamu hubakishiwa
03fe172fff231e0d8a209263a1e8e098.jpg

Ndio maana hasahau kula
Ndio maana mwili ukichoka atapumzika
Ndio maana usiku ukiingia atalala
Ndio maana hachani hela wala kutupa
Ndio maana akivuka barabara lazima achukue tahadhari japo si kwa asilimia mia moja
Ndio maana huhisi kupendwa ama kuchukiwa nknk
Yote kwa yote kuna jambo kubwa nyuma ya vichaa ambalo huwa hatujishughulishi nalo zaidi ya kuwa na mawazo hasi kila tuwaonapo!
fef750dd34a4c90eb777e8e0fdeeafb3.jpg



Sent using Jamii Forums mobile app
Mshana hii ni wapi?
 
Ni mawazo tu! Kichaa ni kupungua kwa Uwezo wa akili ya kawaida kuzuia fikra za kimawazo kuwa matendo kamili yasiyoonekana huku muhusika akiamini yanatendeka na kuonekana.

Khali hii, huvikuta viumbe vyote haswa aina ya wanyama.Ndo maana wakati mwingine binadamu anawaza mambo kwa kuyatengeneza yy mwenyewe na kuyafurahia/kuyachukia na akishindwa kujizuia atatoa sauti/kukimbia/kukaba.
Au kufanya tendon lolote lisilo la kawaida machoni pa watu.

Khali hii ikiwa na muendelezo wa Siku kwa Siku MTU huyu au kiumbe hiki huitwa kichaa,hivyo kila MTU ni kichaa kwa kiasi Fulani maana hakuna asiye na fikra za kimawazo zisizotendeka kuwa matendo kamili.huku yy mwenyewe akifurahi au kuchukia au kukimbia au kutabasamu.
 
Ni kweli kitabu cha UFUNUO ni dilutional thoughts za muandishi?! kwamba aliyokuwa akiyasimulia ni yeye tu aliyaona, na ni vitu vya kufikirika tu. Je Unaamini anaweza kuwa alikuwa KICHAA a.k.a MWEHU
Hapana hakuwa delusional labda kama unamsoma juu juu na huelewi... Ukiangalia anapoongelea kuhusiana na mpangilio wa namba, nyota na vitu na ukafananisha na yale yanayotokea na kufanyika sasa ukimwenguni hasa kwenye level za kimason utaona ule ni ufunuo mkubwa... Ngoja nina mada yake nikiipata takualika
 
Ni kweli kiongozi..mimi pia nishaona watu wengi wakiwanyanyasa na kuwapiga wenye matatizo ya akili...Mungu awalinde waja wake hawa..nawahurumia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeyote anaye mnyanyasa kichaa na yeye anatakiwa apimwe akili, unaweza kumkimbia kwa matendo yake unapokutana naye barabarani na si kumpiga au kuonyesha humpendi, Ni binadamu yule na hujui sababu ilyompelekea kuwa hivyo, huwa nawahurumia sana hao watu
 
Back
Top Bottom