Vichaa wawili walilazwa, sasa pale wodini wakajadili jinsi ya kutoroka pale wodini. Wakaafikiana kwamba wakifika getini wampige mlinzi, mlinzi akikimbia wao watoke nje ya geti kisha watoroke. Wakaondoka wakaenda hadi pale getini, walipofika pale wakakuta geti lipo wazi ila mlinzi hayupo. Wakanong'onezana "dah! Dili limeharibika mlinzi mwenyewe hayupo" kisha wakarudi tena wodini!
hao ndo hamnazo!!Wavuta bangi wawili walikuwa wanaangua maembe kwa mawe yakawa hayadondoki mmoja akamwambia babuu eeeeh ngoja nipande juu nikayacheki vizuri akapanda akayaangalia na kukuta mawili yamelegea akashuka na kumwambia mwenzake oyaaa eeeeeh yameshalegea bado kidongooo tu yataanguka tuendelee kurusha mawe wakaendelea kurushia mawe