Vichekesho vya TFF na Play-Offs za Daraja la Kwanza

Kiukweli bodi ya ligi wanatakiwa waboreshe kidogo tu maana ukisema timu za ligi kuu zicheze na za daraja la kwanza utegemee wa daraja la kwanza kushinda ni vigumu sana.
Mfano mzuri upon kwenye FA angalia kama kuna timu ya daraja la kwanza ambayo imewahi fika hata nusu fainali ?
Kwanini timu za daraja la kwanza zianzie nyumbani zote?
 

Haupo sahihi.
Usahihi ni kwamba anayemaliza wa kwanza kwenye groups za daraja la kwanza ndio anapanda moja kwa moja.

Wanaoshika nafasi ya pili na ya tatu kwenye kundi moja wanacheza play off na na wenzao walioshika nafas kama hizo kwenye kundi jingine. Washindi ndio wanacheza play off ya mwisho na timu kutoka TPL.

Kwa hiyo hapo utaona Pamba kabla ya kucheza play-off na Kagera alicheza kwanza playoff na Mbeya Kwanza.
 
Acha ubishi timu mbili zilizopanada ligi kuu toka ligi daraja la kwanza ni Namungo fc na polisi, zilizoshika nafasi ya 3&4 ndio zimepambana na mwadui na kagera. Hii ipo sahihi kabisa kibonde ligi kuu apambane na anaetaka kupanda wa tatu na nne sio waje watoe point za bure km african lyon
 
Rejea mfumo wa England.
 
Kuwa mbishi nayo inaruhusiwa.
 
 
.

Dah! tunabishana jambo dogo sana nimekwambia haupo sahihi namaanisha Namungo iliongoza kundi B na Polisi Tanzania iliongoza kundi A. Hakuna mshindi wa pili hapo.

Play off zilicheza Pamba iliyoshika nafasi ya tatu kundi A vs Mbeya kwanza ambaye alikuwa mshindi wa pili kundi B.

Then Geita gold alishika nafasi ya pili kundi A akacheza na JKT mlale aliyeshika nafasi ya tatu kundi B.

Tatizo ligi daraja la kwanza haifuatiliwi sana.
 
nimehuzunika sana kwa geita kutokufuzu.
 
Then unaonyesha hukuwa unafuatilia ligi daraja la kwanza ndio maana unadhani ligi ilikuwa na kundi moja.
 
Kiuhaliaia si Dhanj kama ni sawa..inabidi huu utaratibu uangaliwe..ikiwezekana kama utashindwa kubadishwa..timu zicheze play off kwenye neutro ground
 
Kagera haikucheza na timu hizo za Yanga, Simba na Azam?
Matokeo yake?
 
hivi kama hiyo pamba kwa mfano imeshindwa kwa kagera sugar ambayo ni kibonde ligi kuu unategemea ipewe nafasi ili ije icheze na simba, yanga au uzam?
Hapa ndio umeharibu kabisa!! Kwani hujui kuna dirisha la usajili na maandalizi kabla ya ligi kuu kuanza..... Lazima wangesajili wachezaji na makocha wenye ubora ili timu iwe na ushindani mfano wolves kma ingecheza playoff last season isingepanda maana haikua na timu ya kupambana ligi kuu ila wote tulishuhudia dirisha kuu walisajili wachezaji wengi sana na imefanikiwa kuingia top 6 ya EPL.

So hii hoja yako haina mashiko kwamba kufungwa wakiwa daraja la kwanza basi hawawezi kuifunga simba msimu ujao wakiwa ligi kuu.
 
Huu mfumo haupo fair kwa timu za daraja la kwanza. Timu yoyote ya ligi kuu ina wachezaji wa viwango vya juu kuliko hawa.

PL timu inapopanda huwa inapewa around paund 70m ili iweze kusajili na kuhimili ushindani wa PL.

Huku timu zinazoshuka zinatakiwa kuwapunguza wachezaji wakali/wenye gharama ili iwe na uwiano wa kiushindani na timu za championship. Sidhani Kama tff hii inauelewa wa playoffs na chimbuko la ffp
 
Ligi yetu hasa ya daraja la 2 timu zina uwezo mdogo sana.. uwanjani hadi mfukoni.
Ndio maana zikipanda Ligi kuu zinatakiwa kukusanya players wa kuwapush angalau wasalie Premier.. wakikosea kuchanga karata zao vzr lazima washuke daraja.
Mfumo huu wa TFF unazibeba timu za ligi kuu zinazotakiwa kushuka daraja,.[ILA NI MZURI KAMA DARAJA LA KWANZA INGEKUWA LIGI BORA YENYE MAPATO MAZURI.]
Timu 2 zimepanda direct, kweli kuna haja ya timu hizi kucheza wao kwa wao, hawa wa ligi kuu washuke tu.
 
Hata mimi bado sijaielewa tiefuefu yaan uliona wapi timu inashuka ligi uku inakuja chini inacheza mechi mbili inarudi ligi uku tena msimu huu huo daaaah ndio maana kila nikifatilia vya nyumbani ulaya pananivutia narudi
 
Nitajie nchi mbili zinazotumia mfumo huu
 
Yeeess.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…