Crispin Nyoni
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 413
- 90
Jamani niko ugenini wenyeji wangu wamepika vichoma nguo kabla havijaota miba vikiwa vidogo sana wamekatakata kama mchicha wameunga kwa karanga. Je nile ni salama kwa afya?
Ndio tatizo lenu kuzoea chips mayai, ------- kabisa! Hio ni mboga Tamu sana lazima nikienda home Mama yangu aniandalie na nyanya chungu kwa ugali lainiiiii. Ndio maana akina Elli wetu hawahitaji kunywa supu ya pweza!!!!!
Vichoma nguo ni vitu gani tena Bajameni?
tuwekeeni picha basi
Jamani niko ugenini wenyeji wangu wamepika vichoma nguo kabla havijaota miba vikiwa vidogo sana wamekatakata kama mchicha wameunga kwa karanga. Je nile ni salama kwa afya?
Kama unawasiwasi, subiria waanze kula, ikipita kama dakika kadhaa hivi hawajadhurika na wewe kula!
Mkuu natumia "like" ningegonga "simu". Umekuta wenyeji wako wanakula ingekuwa na madhara ungewakuta? Bibi yangu aliniambia kuwa inatibu hadi vidonda vya tumbo na inakausha vidonda haraka sana. Unapokea mgeni kama huyu balaa.
Wageni wengine tabu sana. Umekuta wenzio wanakula na wewe kula tu hapo kibaya kiko wapi?. Argh!