Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri kwa kutoa maagizo yanayoliondoa Taifa kwenye kutumia mabavu na kujielekeza kwenye kutumia akili katika ukusanyaji kodi bila kuathiri walipakodi.
Mbali na hivyo, Nape alisema pia Rais Samia ameonyesha nia ya kuliongoza Taifa kwa kuwatendea haki Watanzania, hasa alipoitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuziangalia na ikiwezekana kuzifuta kesi zisizo na msingi wala uhalali ili kuleta haki.
Mwezi mmoja uliopita usinge thubutu kusoma Nape amchambua Rais John Magufuli.