Vicky Kamata aokoka

Vicky Kamata aokoka

tuombe mungu maana siku hizi waliowengi wanatangaza kuokoka, wasiwasi wangu je wameokoka kweli??? maana miezi mitatu ya mwanzo utawapenda ila baada ya hapo duh ni tofauti na walokole. Tumuombe mungu

Jamani ukianza hoji dhambi za mwenzio kwanza tazama zako. Huyo mdada kama kasema anampenda Yesu akimanisha kaokoa ni yeye kwani uokovu ni matendo sasa katangaza mbele ya viumbe tumesikia lakini siri kubwa moyoni mwake na mungu amsikilizaye ushuhuda wake kama kweli kaachana na yote katika amri 10 za mungu hongera zake la kama ataendelea na mkwere kazi kwake atazidisha bifu na mwalim watapambana kwani mungu uwa hamfichi mnafiki. Na hata huo wimbo ukiusikiliza kwa akili tayari kamfumbia mwalim yeye amsifu kristo tu fumbo za kiivyoo hazina mana tena ujumbe kwa mwalim ampelekee kwa njia nyingine co kupita wimbo huo!

tunamtakia amani katika maisha ya kristo mwokozi wetu, ALELUYA!

ILA TUPO WENGI TULITANGAZA HIVYO LEO HII Mmmmmmm!!!

Kama ni muongo nafikiri Mungu ana uwezo wa kuchapa viboko wanaotumia jina lake Kufanya upumbavu. tatizo lletu sisi watanzania au binadamu tunapenda kuangalia ya zamani. Kama nimefanya mengi mabaya nimeamua kumrudia Mungu nihesaibie kuanzia pale niliposema nimeokoka. Ila wokovu si mchezo, anahitaji kuomba sana hiivi ndimi za watu zinanena!

Tumtakie kila la kheri!

Ni bahati mbaya uokovu unatafsiriwa kutoka maisha ya mtu yaliyopita, na kibaya zaidi mtu akiokoka watu wnafikiri amekuwa malaika, watu wate jueni kuokoka ni hatua ya kumkiri MUNGU kuwa bwana na kiongozi wa maisha yako na ni hatua ya kwanza ya kumkaribisha MUNGu kuishi nawe ni hatua muhimu sana, lakini unongeka na mumfahamu MUNGU na ukuu wake kadri unavutia juhudi katika kumtafuta kupitia neno na mafundisho yake.

Mtu kuanguka ni jambo la kusikitisha lakini linawezekana kama mtu hakupata Muda wa kuongeza ujuzi katika MUNGU, penginepo watu wasichukulie uokovu ni jambo rahisi na kuwa katisha tamaa watu wanpoamua kuja kwa YESU, tutiane MOYO kwani safari ni njema na mapita yake yanawezekana tofauti na watu wengine wanavyo wahukumu watu na matendo yao ya awali. Tusimpe shetani nafasi ya kutesa watu, je si bora mtu akija kwa MUNGU kuliko kubaki kwa shetani?

Nani aliye okoka hakuwa mwovu? au nini amtumikiaye shetani sasa na ni matakatifu?. ikiwa hakuna basi watu wafanyapo maamuzi mema tuwatie moyo na tusiangalie kesho, kwni kesho ni ya MUNGU.

Huyu dada si nasikia ni mke wa ******? Au habari hizi sio za kweli! Hawezi kusema ameokoka na anampenda Yesu then mjengoni anaishia kushadidia ufisadi wa chama kilichomuweka mle ndani mjengoni. Huo ni uongo. Unajua hawa wanasiasa vijana ni wepesi wa kujifunza na kuga mikakati ya waliowaweka na kuwaingiza kwenye siasa. Ufahamu wangu ni kuwa huyu mdada ni mbunge wa viti maalumu ca chama cha magamba, ni vipi ataweza kujisafisha na hayo magamba na wakati huo huo akasema ameokoka. Hiyo ni janja ya kupata kura za 'wapendwa' 2015 atakapoamua kugombea kwenye jimbo. Si mnajua hicho ni kiburudisho kingine cha ******???? Hakuna kitu hapo ni siasa tu inayomsumbua.

Napita tu wakuu, nisalimieni wote!!!!!!!!

Zilikuwa ni habari za uvuguvugu nilizokuwa nazisikia bila kuamini, ila jana alithibitisha mwenyewe pale alipouulizwa na mtangazaji Rita wa Praise power pale Diamond Jubilee kama ni kweli ameokoka au lah!! Vick alijibu hivi " Yes!! nampenda Yesu"

kuthibitisha hayo aliimba kibao chake kinachooitwa yakale yamepita katika mashairi ya wimbo wake kuna maneno yanayosema hivi" kama mfalme ameshanisamehe ww ninani unayeendelea kunisumanga? unayeendelea kunisema vibaya?? yakale yamepita!!!

Ni wimbo mzuri na wenye kuvutia!!

Tumuombee Mungu, asonge mbele, ampigishe hatua zaidi, na awe mfano kwa wengine!!

Susy, Rita ( Rita Chiwalo) ni mtangazaji wa WAPO RADIO na si Praise Power.

Kuhusu swali ambalo Vicky kaulizwa na Rita, hakulijibu ila amejieleza kwa jambo jingine. Jibu la swali ilikuwa ni NDIYO au LA ama HAPANA

Ametoka kijasiriamali zaidi. Katika soko la Muziki Tanzania, ule wa Injili unalipa zaidi.

Hajaokoka ktk siku hiyo au kabla labda iwe baada ya siku hiyo. Quote my words.

haya hongera
Zilikuwa ni habari za uvuguvugu nilizokuwa nazisikia bila kuamini, ila jana alithibitisha mwenyewe pale alipouulizwa na mtangazaji Rita wa Praise power pale Diamond Jubilee kama ni kweli ameokoka au lah!! Vick alijibu hivi " Yes!! nampenda Yesu"

kuthibitisha hayo aliimba kibao chake kinachooitwa yakale yamepita katika mashairi ya wimbo wake kuna maneno yanayosema hivi" kama mfalme ameshanisamehe ww ninani unayeendelea kunisumanga? unayeendelea kunisema vibaya?? yakale yamepita!!!

Ni wimbo mzuri na wenye kuvutia!!

Tumuombee Mungu, asonge mbele, ampigishe hatua zaidi, na awe mfano kwa wengine!!

Wacha kumsengenya,kaungana na kina Chidumule.Mzee Makassy.Remmy Ongara(RIP) na wengineo wengi tu,Kupanga ni kuchagua nafikiri kachagua lililo jema mbele ya uso wa dunia.usirudi nyuma dada yetu hata nyimbo zako za kidunia haukuwahi kuimba mapenzi wala matusi nadhani ulikuwa unajitayarisha songa mbele usirudi nyuma utageuka jiwe la chumvi.

Hongera mama. Mungu akulinde na mambo ya dunia.

jamani kama kaokoka au hajaokoka ni yeye na Mungu wake!

Mliocomment mabaya juu yake jitazameni kwanza wenyewe na matendo yenu....

Naungana na waliopongeza.

Hongera kwa kumrudia Muumba wako

Back
Top Bottom