pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 692
- 880
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake laki moja Vicky Kamata amesema Royal tour inaenda kubadilisha akili ya Wanakwake wajitegemee waache kuwa Ombamba. ameyasema hayo Wakati alipokutana na Wanahabari jijini Dar tarehe 20 Mei 2022 kuelezea Madhumuni ya Taasisi ya Wanawake laki moja ambayo ni kupinga Unyanyasaji, Ukatiri na kujengeana Uwezo Kwa Wanawake wote bila kujali Dini, Kabla, Siasa wala rangi.
"Kwenye jamii wanawake bado ni tegemezi. Wanawake wa Tanzania wakichanganyika na Wanawake wa Mataifa Wengine watabadilika akili. Mfano Ukienda kula chakula na Mwanaume, Wanawake wa Tanzania hawachangii Malipo ya Chakula Hotelini kama wenzetu. Hivyo itawafanya wajielewe kiakili na Wataweza kuchangia Bill na ndugu Jamaa na Marafiki kama wenzetu". Wanaume wanasema Chukua namba ya mwanamke, utaifuta mwenyewe kwa jinsi atakavyo kuomba hela. Hatutaki wanawake tegemezi". Amesema Vicky Kamata. Amesema Wanawake wamezoea mwanaume ndo anafanya.
Rais Sama anatakiwa apongezwe na Aungwe Mkono kwa hali na Mali, ni mama shupavu. Mfano Vita vya Ukraine na Urusi, vimepandisha bei ya mafuta duniani sisi sio kisiwa hata Tanzania tumekumbwa na Upandaji wa bei, lakini Rais Samia ameumiza kichwa akachangia Bil 100 kama Ruzuku. Haiingiliani na pesa za maendeleo wala bajeti. Wamejibana sehemu nyingine. Zimbabwe magari yamepaki, sisi tupo na Magari yapo Barabarani. Pamoja na Ruzuku, karuhusu watu wenye uwezo kuleta mafuta. Maghara makubwa ya kuhifadhi mafuta pia yanajengwa. Wanawake tumepata muwakirishi anaye Tujengea kujiamini. Amesema Vicky Kamata.
Wanawake laki moja tupo hapa kuwaunganisha Wanakwake katika mikoa yote ya Tanzania. Rais Samia ni kielelezo cha Ushupavu, Ukakamavu na Uchapakazi, tusibaki nyuma.
Tumuunge Mkono na kumtia moyo.
======
UDHIBITI WA BEI YA MAFUTA NCHINI
Kama mnavyofahamu, hivi karibuni nchi mbalimbali duniani zimekumbwa na msukosuko wa kupanda kwa bei za mafuta kutokana na vita inayoendelea sasa hivi nchini Ukraine.
Tanzania siyo kisiwa na yenyewe pia inakabiliana na changamoto zitokanazo na bei ya mafuta kupanda ghafla kwenye soko la dunia na hivyo kuleta athari katika mfumuko wa bei, gharama za uzalishaji kwenye uchumi na kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi mijini na vijijini.
Kwa ujasiri wa kipekee, Rais Samia ametoa maelekezo kwa semrikali fake kuchukua hatua za dharura kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta duniani kabla ya mwaka ujao wa fedha wa 2022/23.
Badala ya kusubiri hatua za kikodi kwenye bajeti ijayo ya serikali ambayo utekelezaji wake utaanza Julai 1, 2022, Rais Samia ameagiza kuwa ahueni itafutwe mapema zaidi kwa kutoa maelekezo kwamba katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na itolewe ruzuku ya shilingi bilioni mia moja (Shilingi 100,000,000,000) kwa ajili ya kupunguza bei za mafuta hapa nchini.
Kiasi hiki cha ruzuku kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta duniani hakijawahi kutolewa na serikali ya Tanzania tangu tupaje uhuru, lakini kwa ujasiri wa kipekee, Rais Samia ameiagiza serikali Lake kufanya maamuzi hayo magumu ya dharura.
Ruzuku hii inatolewa kwa kupunguza matumizi ya serikali (yaani recurrent expenditure) katika kipindi kilichobaki cha mwaka wa feda wa 2021/22. Fedha za miradi ya maendeleo hazitaguswa na zitaendelea kutolewa kama ilivyopangwa. Ruzuku hii ya shilingi bilioni 100 itatolewa kwa ajili ya kupunguza bei kuanzia tarehe 1 Juni 2022.
Pamoja na ruzuku, Rais Samia ameiagiza serikali yake kuchukua hatua nyingine zisizo za kifedha kuleta ahueni kwa wananchi dhidi ya ongezeko la bei ya mafuta duniani.
Hatua hizo ni pamoja na kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu kufanya hivyo, kuanzisha Mfuko wa Kuhimili Ukali wa Bei za mafuta, Kuanzisha Hifadhi ya Mafuta ya Kimkakati na Serikali kukamilisha makubaliano ya kujenga maghala makubwa ya kuhifadhi mafuta kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kulingana na uhitaji.
Hatua nyingine zinazochukuliwa na semrikali ni pamoja na kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghala moja kupitia maghala ya TIPER ili kupunguza au kuondoa gharama za meli kusubiri au kuchukua muda mrefu katika upakuaji wa mafuta katika maghala mengi, Kuiongezea uwezo TPDC kuagiza mafuta nje ya nchi na Kuimarisha utendaji na weledi wa taasisi za Serikali zinazoshughulika na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja.
Wakati mataifa mbalimbali duniani yamekumbwa na tafrani kutokana na sakata la bei la mafuta, ikiwemo changamoto za foleni na vurugu katika vituo vya mafuta kutokana na uhaba wa mafuta, kumekua na utulivu mkubwa nchini Tanzania, bila uhaba wa mafuta nchini kutokana na hatua za dharura za kijasiri za serikali chini ya uongozi wa kijasiri wa Rais Samia.
Leo hii, mamilioni ya Watanzania wanapata ahueni na wataendelea kupata ahueni zaidi kuanzia Juni 1 na July 1 wakati hatua zisizo za kibajeti na za kibajeti zitakapoanza kuleta matunda.
Sisi Wanawake 100,000 tumezungumza na wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara, madereva wa bodaboda, Bajaj na daladala, mama ntilie na wananchi wote nchini na wote wanaungana kumpongeza Rais Samia kwa ujasiri wa kipekee alionesha katika kukabiliana na tatizo la ongezeko la bei ya mafuta duniani.