Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Victor Makundi amekitaka Chama cha Wanasheria nchini, Tume ya maadili ya Mawakili na Mahakama kuu kutomfumbia macho mwanachama wao Tundu Lissu anayejaribu kuipoka Katiba ya nchi madaraka yake na kuipaka matope na kumchukulia hatua.
Makundi ametoa kauli hiyo leo, alipokuwa akizungumza na vijana 720 wa Chama cha Mapinduzi waliopo kambini wilayani Hai mkoani Kilimajaro ambapo alisema kuwa, haiwezekani mtu mmoja au kikundi cha watu kikawapoka haki ya kupiga kura kwani ni haki ya kila Mtanzania kupiga kura na kuwa na uchaguzi.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Sisi ni vijana wa nchi hii tukishindwa kuisimamia Katiba yetu tukiwa wadogo tunaandaa Taifa gani la kesho ni lazima tusimame imara kuhakikisha katiba yetu inalindwa na haipaswi mtu huyu akaendelea kuachwa akilipotosha Watanzania" alisema Makundi.