Video aliyorusha Miss World kuhusu hali ya umaskini Tanzania; Mama Salma na wenza wa viongozi wa Tanzania bado wanaona ni sahihi kulipwa mabilioni?

Sasa katika hali ya kawaida, Yeye kujenga shule Tz kama malengo yake ya muda mrefu ya kushinda miss world Sisi kama Tz tunapata hasara gani zaidi ya faida ya kujengewa shule?

Aliyeargue hivyo atakuwa kiongozi mwenye wivu kuwa yeye hajafanya chochote na binti wa miaka 18 amefanya kitu.

Na bado this time akija kuleta msaada mwingine atasindikizwa na msafara wa V8 new model kama kumi hivi za viongozi zilizonunuliwa kwa kodi ya mtanzania……

Shame on us!
 
You're stupid
 
Uongozi ni ajira na sio wito, Nyerere alikurupuka kudai uhuru bila kujiandaa.
 
Umasikini wetu ni matokeo ya fikra na sio mazingira.
Hatuna uwezo wa kugeuza mazingira kuwa fursa.
 

😁

Itachukua muda sana Mtanzania kuendelea...

Yaani bado hujaelewa mfano wa jamaa...

Kama mume/mke alikuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na analipwa mafao kwa maisha yake yote, iweje wenza wao wachukuliw3 kama wastaafu wa kitaifa?

Hayo mafao wa waume au wake zao hayawatoshi?
 
Mkuu hata mimi sikubaliani ni hili ila wa kuulizwa ni ofisi ya mwanasheria mkuu, wabunge wote na spika.

Waulizwe, Ilikuwaje wakapitisha sheria ya namna hii. Sisi wadau wa JF tukiulizana humu hata tukakesha hatutapata majibu na wala hatutabadili chochote!

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, je sisi wananchi, walipa kodi na tozo nchi hii, tuliwatuma kupitisha hoja hiyo??

Je wabunge wetu hawa walitushirikisha ili tukubaliane na tujipange namna ya kuwahudumia hao wastaafu wenza kupitia kodi zetu???

Na je katiba inasemaje kuhusu wananchi kuwaadhibu wabunge wanapopitisha hoja ambayo sisi wanachi hatujawatuma wala kushirikishwa?

Bunge ni mahali pa wabunge kupeleka hoja za kutoka kwa wananchi sio za kwao. Shida ni bunge la chama kimoja kupitisha kila jambo bila kushirikisha wananchi au kufanya tafakuri ya kina.

Hii ndio hasara ya uchafuzi uliopita wa Mwendazake! Na bado kuna sheria kibao zenye madhara makubwa kwa wananchi , omba tu yasikukute!

Rais Samia naye mpaka sasa haja batilisha na anaonekana hana nia ya kubatilisha sheria yoyote mbovu iliyopo awali. Badala yake ameweka mazingira laini kwa kutumia mamlaka ya Rais. Akitoka tu imekula kwetu mazima!

Akitokea punguani mwingine akasimamia hizo sheria mbovu japo halali ndio wananchi watajua hawajui!! Na mzunguko wa jenga bomoa, ponya umiza, nenda mbele rudi nyuma utaendelea daima!

Mzunguko mzuri ni wa aina ya spring japo unazunguka lakini unapiga hatua na hata ikatokea umedondoka utanesa.

ila huu mzunguko tuliomo sisi ni duara kavu, kila tukifanya jitihada tunarudi pale pale! Maneno kibao, hatua sifuri!
 
🙏
 
SISI TUKO BIZE KUINGIZA SIASA KWENYE KILA UPANDE, HATA VIONGOZI WANAOTUMWA WAKAPELEKE MAENDELEO, AKILI YAO YOTE INAWAZA KULINDA INTERESTS ZA CHAMA TAWALA.
 
Reactions: Auz
Kama serikali kwa ujumla, ina matumizi ya hovyo tena ya anasa, ilhali wanakwenda kukopa ili kujiendesha, hao wenza hawajali kama serikali na chama chao wasivyojali.
 
ujinga, ubinafsi na tamaa zilizopitiliza zinaanzia hapo kwenye kutumia haki yake vibaya, hyo hoja kuipeleka Bungeni kwake ni kosa kubwa kwenye jamii yenye utambuzi na kujielewa na sababu tosha ya kufanya mamlaka na Taasisi zenye mlengo wa kuendeleza ustawi wa jamii kumulika taa kwa mhusika, ikiwezekana na jamii inayomzunguka kama familia, maana Mtu kama mwanamke kuja na wazo hilo upo uwezekano mkubwa kwamba amejadili na familia yake hususan mmewe. Inasikitisha sana kuwa na jamii yenye watu wenye tamaa iliyopitiliza mkapa shetani mwenyewe analalamika.
 
Wewe ni mjinga kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…