SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

SI KWELI Video: Anayejiita Superwoman akamatwa na mihadarati nchini Oman

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2

Yule Super Women aliyesema anauza Mchicha mpaka Ulaya Leo amekamatwa Oman na Kete 100 za unga.
Screenshot 2025-02-24 220234.png
 
Tunachokijua
Yupo mwanamke anayetambulika kama superwoman (Pendo Open Kitchen”) ambaye amejizolea umaarufu kutokana na vipande vya video vinavyomuhusu yeye akiongelea namna alivyopata mafanikio kutokana na harakati zake ikiwemo kuuza mchicha online hadi mataifa ya nje ikiwemo Uingereza na Ujerumani. Tazama hapa

Madai

Kumekuwepo na kipande cha video kilichoambatana na taarifa kuwa superwoman amekamatwa na madawa ya kulevya Oman. Taarifa hiyo ikihusianishwa na mwanamke aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kueleza kuwa pesa zake anazipata kwa kufanya biashara mbalimbali ikiwemo kuuza mchicha katika mataifa mbalimbali ulimwenguni. Taarifa iliyoambatana na video hiyo inajaribu kuonesha kuwa mwanamke huyo amekuwa akifanya biashara za madawa ya kulevya na hivyo amekamatwa. Tazama hapa na hapa.

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kwa njia ya mtandao na google reverse image search umebaini kuwa video hiyo si ya hivi karibuni. Mttu mmoja aliweka kipande hiko cha video Julai 29, 2023 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram bila kuweka maelezo yoyote yale. Tazama hapa

Ufuatiliaji zaidi umebaini tovuti kadhaa ziliripoti ikiwemo tovuti ya Legit ambayo ilichapisha taarifa Februari 5, 2021 yenye kichwa cha habari “Video inaonesha akiwa na dawa za kulevya zilizojazwa chini ya wigi, maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege wapigwa na butwaa”. Katika Taarifa hiyo walieleza namna tukio hilo lilivyotokea katika uwanja mmoja wa ndege na hali iliyokuwa ikionekana katika tukio hilo ingawa hawakueleza zaidi.

Tovuti nyingine inayojulikana kama Justnaija ilichapisha taarifa iliyoambana na video hiyo tena Julai 23, 2023`ilielezea pia tukio hilo inagwa na wao pia hawakueleza tukio hilo limetokea wapi na ulikuwa ni uwanja upi wa ndege.

Hivyo video hiyo si ya hivi karibuni kama ilivyosambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya kuanzia Februari 21, 2025. Pia hakuna uthibitisho wa kuwa video hiyo inamuhusu Mtanzania.
Its about time kwa Mamlaka kuhakikisha Jamii inapata Role models na Public figures wenye elimu, vipaji vya maana na Kazi za kijasiriamali zenye tija. Muhalifu kama huyu alipataje airtime?? hawa wadada na Wakaka huko social media ambao wana influence upuuzi wanaruhusiwaje kulisha content zao kwa jamii.. ???

Hivi kipindi cha Wasomi, Wagunduzi wa kiteknolojia, Wasanii kutamalaki kwenye vyombo vya habari kiliishia wapi??? Nakumbuka enzi zetu tunakua watu kama Philbert Bay, Tanzania Ones , Doctors, engineers etc ndo vitu vijana walikua wanafuatilia na kutamani.. ila leo Wahalifu wanaruhusiwa kujinadi wazi wazi na kujipa majina ya sijui wapambanaji, content creator, social media figures na takataka zingine.. jaman Sera zitungwe ili kuokoa jahazi.. social media Contentz zinanguvu kubwa sana kushape direction ya Jamii nzima.. watu kama hawa wasipewe Nafasi kabisa..
Unaweza kushangaa hawa watu wasioleweka hata biashara zao hazieleweki ndio wanapata airtime ..Kuna yule chief wa Mbeya yaani hovyo kabisa.
 
Yaan hizi mbuzi, na wasanii hawa Akina Chino, Nifah ,wale Ma DJ ,wasanii wanaojificha CCM.

Unajiuliza, huyu Chino kama kudensi Kuna Akina Iyobo wameanza kitamboooo, inakuaje kuaje??.

Kama uDJ unajiuliza, mbona MaDJ ni wengi sana, inakuaje MTU ana nyumba ya B 1+, Magari ya kifahari

Kiukweli kabisaaa kabisaaaa, Hapa Bongo, Sanaa ya Muziki, Filamu, Uchekeshaji, Biashara mitandaoni , Badoo haijafikia Hadhi ya kumpa MTU Nyumba za Mabilioni Kadhaa ,Magari ya mabilioni .

Badoooo, badooooo !!!.

Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao
"Manina zao, wanatupa stress tukidhan tumechelewa kumbe ndo zao "🤣🤣
 
Kwa waarabu kaisha huyo ,halafu ni ushamba sana yaani hapo hata zile Scanner za screening airport anashikwa.
Sijui alidanganywa na nani kuweka sumu kichwani wakati sasa hivi wakichukua picha inaonyesha kila kitu aisee yupo mwingine dada kutoka SA alikamatwa Hong Kong yeye alisukia kwenye rasta zilikatwa rasta zote ndio wakachambua sumu..
 
Its about time kwa Mamlaka kuhakikisha Jamii inapata Role models na Public figures wenye elimu, vipaji vya maana na Kazi za kijasiriamali zenye tija. Muhalifu kama huyu alipataje airtime?? hawa wadada na Wakaka huko social media ambao wana influence upuuzi wanaruhusiwaje kulisha content zao kwa jamii.. ???

Hivi kipindi cha Wasomi, Wagunduzi wa kiteknolojia, Wasanii kutamalaki kwenye vyombo vya habari kiliishia wapi??? Nakumbuka enzi zetu tunakua watu kama Philbert Bay, Tanzania Ones , Doctors, engineers etc ndo vitu vijana walikua wanafuatilia na kutamani.. ila leo Wahalifu wanaruhusiwa kujinadi wazi wazi na kujipa majina ya sijui wapambanaji, content creator, social media figures na takataka zingine.. jaman Sera zitungwe ili kuokoa jahazi.. social media Contentz zinanguvu kubwa sana kushape direction ya Jamii nzima.. watu kama hawa wasipewe Nafasi kabisa..
Mkuu, kuwa-control hawa watu ni ngumu sana kwa sasa hivi kwa sababu ya social media na soko huria la vyombo vya habari. Huoni sasa hivi makahaba kama kina Mobeto ndiyo wamekuwa gumzo na ''mfano'' kwa jamii? Kila anapobadilisha mwanaume ndivyo anavyoshangiliwa. Njia sahihi ni wewe kufunza watoto na watu wako wa karibu ili wasiwe wafuata mkumbo. Wajitambue, wajiamini na kujikubali.
 
Ng
Ipo kee utakavyo ipokea ila ameanguka akitafuta.

Cha msingi kufanya kazi hakuna ubishi hapo ni

Subiri anyanyuke then atakuja kukusimulia namna ambavyo biashara halali ya mchicha ingemlipa endapo angeamua kutumia akili na nguvu kuliko kutanguliza tamaa ya pesa za haraka.. yaan huna hata akili za kawaida unaenda kufanya biashara inayo hitaji zaidi ya elimu ya Chuo kikuu?? Alafu unajiita mpambanaji… fool!
 
Mkuu, kuwa-control hawa watu ni ngumu sana kwa sasa hivi kwa sababu ya social media na soko huria la vyombo vya habari. Honi sasa hivi makahaba kama kina Mobeto ndiyo wamekuwa gumzo na ''mfano'' kwa jamii? Kla anapobadilisha mwanaume ndivyo anavyoshangiliwa. Njia sahihi ni wewe kufunza watoto na watu wako wa karibu ili wasiwe wafuata mkumbo. Wajitambue, wajiamini na kuwa na kujikubali.

Mkuu inawezekana mnoo wala hata sio kwa kutumia Nguvu nyingi.. maana hao wanaopost wanajulikana ni swala la kitaaluma tu, ita hao watopotoshaji wape elimu kidogo, vyombo vya habari vipewe jukumu la kuelimisha umma kuhusu hilo swala kama ambavyo wanatangaza matangazo ya kubet 24/7 watu wenye elimu na vipaji vyenye Tija ndo waanze kuitwa kwenye National Functionz etc Vipindi vya tv, redio yaan mkiamua kusafisha akili za watu ni miezi sita tu.. inabaki historia
 
Ng

Subiri anyanyuke then atakuja kukusimulia namna ambavyo biashara halali ya mchicha ingemlipa endapo angeamua kutumia akili na nguvu kuliko kutanguliza tamaa ya pesa za haraka.. yaan huna hata akili za kawaida unaenda kufanya biashara inayo hitaji zaidi ya elimu ya Chuo kikuu?? Alafu unajiita mpambanaji… fool!
Huo muda wa kusimulia ataupata wapi?
Ashaenda huyo + age yake ni mbibi akitoka
 
Back
Top Bottom