Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Iliishaje?Video ikimuonyesha askari akivutana au unaweza kusema kupigana na mmoja ya mwanachi.
Watu waliokuwa eneo la tukio wanahoji kwani amefanya kosa gani lakini bado polisi hao wawili walikuwa wanalazimisha mwananchi huyo kuingia kwenye gari lao.
View: https://www.instagram.com/reel/Ddl-1EYoPsD/?stkn=MTNwbnN3azM1c2N6bA%3D%3D
Nawakumbusha tu kwamba mazoezi ni muhimu sana. Mtu mwenye afya njema na utimamu wa mwili huwa na nguvu, stamina na uwezo wa kujilinda zaidi. Ni vigumu sana kupelekeshwa au kuvutwa-vutwa kirahisi na polisi bila yeye kuwa na uwezo wa kujitetea.
Tujenge afya zetu mapema—mazoezi si kwa ajili ya mwonekano pekee, bali pia kwa ajili ya nguvu, afya na uimara wa mwili.
Umesahau Jeshi jktkipindi nipo mdogo hawa watu wa sare tuliogopa hata kupishana nao heshima tuliwapa
wakaanza walimu wakashiriki ujinga na wizi tukawadharau hivi majuzi hawa nao wakashiriki tena waliingia vibaya kwelikweli
Leo? Heshima imepotea
Yeyote atumiwae huishia katika aibu kuu