Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameonekana akiwa katika hali ya furaha kubwa kanisani kwake, akicheza na kuimba pamoja na waumini, ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana kanisani hapo baada ya kanisa hilo kufunguliwa.
Kanisa hilo lilifungiwa kwa muda na Serikali kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji wa taasisi za kidini, baada ya Askofu Gwajima kukosoa masuala ya Utejaji, Utawala bora, masuala ya uchaguzi, jambo ambalo lilielezwa kuwa linakiuka sheria na kuhatarisha utulivu wa jamii
Soma pia PreGE2025 - Askofu Gwajima: Utekaji si utamaduni wetu na halitakiwi kuchekewa!
Serikali kupitia Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, ilitangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima, kuanzia Juni 2, 2025.
Hatua hiyo ilichukuliwa siku moja baada ya Gwajima kutangaza msimamo wake wa kuendelea kukemea vitendo vya utekaji na watu kupotea.