Asante mmwanakijiji, je ni wapi ninapoweza kupata mkanda mzima?
Ahsante MMKJ, naungana na jamaa hapo juu, kila utamu unapokolea clip inakwisha, wapi tunaweza kupata makanda kamili.
Niliangalia mahojiano na ITV [Renfred Masako] wiki iliyopita, Dr Slaa alikuwa anajibu maswali yanayohusiana na sera za Chadema, kwakweli anaielewa vema sera za chama chake. Yaani akiongelea afya utapenda, akiongelea elimu utapenda, haongelei vituo vya afya au shule moja ya msingi anaongelea kwa ujumla wake kwa kina na mantiki. Nilikuwa nyumbani kwa mjomba wangu ambaye ni CCM kiaina, baada ya mdahalo ule alisema '' mtu anyeongelea kitu kinachoitwa ilani ya uchaguzi kwa maana yake halisi miongoni mwa wagombea wote ni Dr slaa''. Nikamuuliza ni kwanini , akajibu anamwelewa kama alivyokuwa anamwelewa mwalimu Nyerere. Nikamuuliza je unamkubali, akasema hana shaka na uwezo wake,anashaka na watakaomsadia.
Huyu Dr, tukubaliane kutokubaliana anaongea kwa data na anajua anaongelea nini, labda mshindani wake ni Lipumba, lakini JK afadhali amekacha na aendelee kupandisha vituo vya afya hadhi za hospitali za rufaa hata kama hakuna wataalamu na vifaa.
Ni aibu kubwa rais wa nchi kama tanzania aongelee ujenzi wa flyovers za tazara na ubungo,hiyo kama alivyosema Slaa ni kazi ya halmashauri za miji na mameya wao, rais anatakiwa aongelee infrastructure za nchi kwa ujumla.
Lakini kinachoniudhi zaidi na kampeni za CCM ni kuwatumia walemavu wa viungo. JK kila anapokwenda eti lazima aongee na mlemavu mmoja ili kujenga taswira ya kujali. Miaka 5 iliyopita hatukuona akiinama kuongea nao na kama alifanya hivyo aliwasaidiaje. Kuwatumia walemavu kutafuta kura ni dhambi kubwa. Tuwasaidie wenzetu kwa huduma muhimu na si kutafuta kura.Tumuogope mungu jamani.
Watanzania sikilizeni sera na hoja na si rangi wala kofia na vitenge.