Elections 2010 Video Chache za Mdahalo wa Dr. Slaa ITV

Ahsante sana Mwanakijiji, walau na sisi ambao hatukupata nafasi ya kushuhudia live tumeweza kupata vionjo kidogo. Ila hiyo clip ya mwisho imegoma kucheza. Halafu hizo nyingine zinaishia katikakati kiasi ambacho ladha yake inatibu. Hope utaweza kulifanyia kazi.

Otherwise this is great and I am sure were are getting there soon..!
 
Mwanakijiji you're best!...mwache JK azidi kujisifia kuwa ni 1st president kuonana na Obama wakati wanaume wanaweka mikakati ya kuwezesha watanzania waliokosa matumaini na serikali ya ccm+wahindi wasio na chembe ya uzawa bali kuimaliza nchi.
 
nimeelewa kwa nini jk alichomoa mdahalo, mzee kwa nini nchi yako maskini?mimi sijui Slaa angemgaragaza vibaya kihiyo jk
 
Asante mmwanakijiji, je ni wapi ninapoweza kupata mkanda mzima?
 
Shukrani Mwanakijiji kwa video,
Pia mdau Mzozaji ametupatia linki ya mdahalo wa Dr. Slaa Ph.D ktk mfumo wa audio wenye urefu wa takribani saa 1 na dakika 25 (yaani jumla ya dakika 85) za maongezi ya Dr. Slaa na Watanzania siku ya jumamosi 23/10/2010 : sikiliza hapa http://www.chirbit.com/mambo mdahalo mzima.
 
Kichuguu ninayo audio karibu yote.. nitawapandishia kesho....
 
Nilishangaa sana maana wengi wameuliza maswali mepesi, kulikuwa na maswali makubwa zaidi ya kumuuliza Dr.
 
Asante mmwanakijiji, je ni wapi ninapoweza kupata mkanda mzima?

Ahsante MMKJ, naungana na jamaa hapo juu, kila utamu unapokolea clip inakwisha, wapi tunaweza kupata makanda kamili.
Niliangalia mahojiano na ITV [Renfred Masako] wiki iliyopita, Dr Slaa alikuwa anajibu maswali yanayohusiana na sera za Chadema, kwakweli anaielewa vema sera za chama chake. Yaani akiongelea afya utapenda, akiongelea elimu utapenda, haongelei vituo vya afya au shule moja ya msingi anaongelea kwa ujumla wake kwa kina na mantiki. Nilikuwa nyumbani kwa mjomba wangu ambaye ni CCM kiaina, baada ya mdahalo ule alisema '' mtu anyeongelea kitu kinachoitwa ilani ya uchaguzi kwa maana yake halisi miongoni mwa wagombea wote ni Dr slaa''. Nikamuuliza ni kwanini , akajibu anamwelewa kama alivyokuwa anamwelewa mwalimu Nyerere. Nikamuuliza je unamkubali, akasema hana shaka na uwezo wake,anashaka na watakaomsadia.
Huyu Dr, tukubaliane kutokubaliana anaongea kwa data na anajua anaongelea nini, labda mshindani wake ni Lipumba, lakini JK afadhali amekacha na aendelee kupandisha vituo vya afya hadhi za hospitali za rufaa hata kama hakuna wataalamu na vifaa.
Ni aibu kubwa rais wa nchi kama tanzania aongelee ujenzi wa flyovers za tazara na ubungo,hiyo kama alivyosema Slaa ni kazi ya halmashauri za miji na mameya wao, rais anatakiwa aongelee infrastructure za nchi kwa ujumla.
Lakini kinachoniudhi zaidi na kampeni za CCM ni kuwatumia walemavu wa viungo. JK kila anapokwenda eti lazima aongee na mlemavu mmoja ili kujenga taswira ya kujali. Miaka 5 iliyopita hatukuona akiinama kuongea nao na kama alifanya hivyo aliwasaidiaje. Kuwatumia walemavu kutafuta kura ni dhambi kubwa. Tuwasaidie wenzetu kwa huduma muhimu na si kutafuta kura.Tumuogope mungu jamani.
Watanzania sikilizeni sera na hoja na si rangi wala kofia na vitenge.
 
Nisaidieni WanaJF PC yangu haisomi hizo picha/video naona kisanduku na kitu kidogo pemmbeni kushoto. hii ni nini tatizo. Asante
 
Hamna lolote pale, ni clip mojawapoa ya video za hapo juu ndiyo aliyo rip audio channel.
Well done. Nimeipata vizuri. Tunatarijia uadilifu, uwajibikaji na urejeshwaji wa nchi katika hali ya kawaida.
 
Kaka M. Mwanakijiji asante sana, hebu fanya jitihada kwani kuna watu wanataka Tape yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…