Binamu wa rais wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad aliukiwa kwa kunyongwa na baada ya kupandishwa juu na crane.
"Baada yakuwasili kwa vikosi vya waasi wa Syria katika mji wa Latakia, ilitangazwa kuwa Suleiman al-Assad, ambaye alikuwa kiongozi wa Vikosi vya Ulinzi wa Kitaifa, aliuawa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Suleiman al-Assad alinyongwa kwa kutumia kreni katika uwanja mmoja huko Latakia. Sababu ya kuuawa kwake ilikuwa uhusiano wake wa damu na rais wa zamani, pamoja na "uhalifu dhidi ya wale waliopinga utawala huo."
"Baada yakuwasili kwa vikosi vya waasi wa Syria katika mji wa Latakia, ilitangazwa kuwa Suleiman al-Assad, ambaye alikuwa kiongozi wa Vikosi vya Ulinzi wa Kitaifa, aliuawa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, Suleiman al-Assad alinyongwa kwa kutumia kreni katika uwanja mmoja huko Latakia. Sababu ya kuuawa kwake ilikuwa uhusiano wake wa damu na rais wa zamani, pamoja na "uhalifu dhidi ya wale waliopinga utawala huo."
- Tunachokijua
- JamiiCheck imefuatilia kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kikimuonesha mtu amening’inizwa/ananyongwa na madai ya kuwa mwanaume anayeonekana katika video hiyo ni binamu wa aliyekuwa rais wa syria ambaye amepinduliwa tarehe 8/12/2024 na kubaini kuwa video hiyo inayosambaa pamoja na ujumbe wake inapotosha kwani video hiyo haihusiani na binamu wa Bashar. Tazama taarifa hiyo hapa na hapa.
Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao imebaini kuwa video hiyo iliwekwa mtandaoni tarehe 7/12/2024 katika mtandao wa facebook katika akaunti ya ‘ حكي حوراني’ kwa kiingereza ni Hawrani story ambapo pamoja na video hiyo waliambatanisha video nyingine pia huku zikiambatana na ujumbe kuwa ni tukio la kunyongwa kwa watu hao wanaohusishwa na mauaji ya kijana ‘Hajj Ali’ katika eneo la wazi katika mji wa Khurba Ghazaleh, Daraa Syria.
Video ya kwanza (The first part) ilikuwa ikimuonesha mwanamke ambaye kwa mujibu wa حكي حوراني wameeleza kuwa mtu huyo alijulikana kwa jina la Diana akiwa ananyongwa kutokana na jambo hilo.
Video ya pili (The second part) inaendelea kuonesha tukio la Diana kuanzia mwanza alipokuwa anaandiwa kwa kufungwa kamba kwa ajili ya zoezi hilo, video hiyo imeambatana na ujumbe unaoeleza kuwa Daina alikuwa ni mke wa.
Video ya nne ambayo ndiyo haswa inahusianishwa na kunyongwa kwa kwa binamu wa Bashar al-Assad waliyemtambulisha kwa jina la Meja Jenerali Suleiman Hilal al-Assad, inamuonesha mwanaume mmoja akiwa amening’inizwa juu huku kukiwa na umati mkubwa watu ukishudia tukio hilo. Ambaye kwa mujibu wa post ya حكي حوراني wameambatanisha ujumbe unaoseomeka;
''Kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa "Amar Al-Saad" katika uwanja wa umma katika mji wa Kharba Ghazaleh katika mashamba ya Daraa Mashariki, ili kulaani kosa la kumuua kijana "Mohammed Ziad Al-Hajj Ali". baada ya kukamatwa baada ya kuchukua udhibiti wa gereza la Jiji la Izra lililopo katikati mwa Daraa mashambani''
Hivyo video inayohusianishwa na tukio la kunyongwa kwa binamu wa Bashar inapotosha kwani mwananume aliyekuwa akinyongwa katika tukio lile حكي حوراني wao walimtambulisha kama Suleiman Hilal al-Assad.
Tovuti ya uhakiki wa taarifa ya DFFRAC ORG katika ufuatiliaji wake ilibaini kuwa taarifa ya tukio hilo la kunyongwa kwa mwanamke na mwanaume huyo liliripotiwa katika tovuti ya Daraa24.org ambao walieleza kuwa kwa mujibu wa mwandishi wao; hukumu ya kifo ilitekelezwa dhidi ya “Ammar Al-Asaad” na “Diana”, mke wa mwanaume aliyeuawa “Mohammad Ziad Al-Hajj Ali, Abu Ayser”, kwa hatia ya kutekeleza mauaji ya kijana Al- Hajj Ali. Taarifa hiyo iliwekwa katika tovuti ya Daraa24.org ilitolewa tarehe 07/12/2024 na imehifadhiwa hapa.