Video: Dereva wa Lori akutwa amekufa kwenye cabin ya gari huko Mukambo

Video: Dereva wa Lori akutwa amekufa kwenye cabin ya gari huko Mukambo

Hii inshu ya sumu imekaaje wakuu..nasikia madereva wanakufa sana.
 
Nime Google ni mpakani mwa DRC na Zambia upande wa DRC

Kwa kuitizama video, Haiwez kuwa congo hapo,
1.uniform za polisi wa zambia
2. plate number kwenye gari ndogo ni ya Zambia pia
3. Wanasikika wakizungumza Bemba (Ligha ya Zambia) na kiswahili chenye lafudhi hiyo pia kwa baadhi ya wazungumzaji.
 
Makambo ndo mtaa gani hapo Dar?
Sie wengine ni wageni
 
1, dereva anaweza beba mzigo wenye kemikali au sumu, halafu analala kwenye cabin, ile sumu inamuua taratibu usingizini.

2, dereva Kila sehemu akisimama anakula kitu, anaweza kula sumu bila kujua.

3, mmiliki wa gari ameizindika gari yake kuipa ulizi, dereva nae anaenda kujizindika kujipa ulinzi binafsi, mambo yakikutana dereva anazidiwa na kupoteza maisha.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app


4; Muumba wa vyote ameona muda wa dereva kuwepo duniani umeisha, kazima data.

5; Dereva alikua anaumwa magonjwa sugu ya muda mrefu.

6; Dereva amepatwa na mshituko wa moyo kwa ghafla ikapelekea umauti wake.

7; Baadhi ya madereva wanamiliki nyumba ndogo kila kituo, itafutwe pisi yake ya hicho kituo.

8; Zamu yake.
 
Dereva wa Lori Mtanzania akutwa amekufa kwenye cabin ya gari yake huko Mukambo.

Alikuwa anaendesha gari yeye namba za usajili T 692 EDC mali ya kampuni ya Inara Investments( Tanzania) Ltd.

Mwili wake umehifadhiwa polisi Mukambo border kwa ajili ya kuwatafuta ndugu na jamaa zake .

Video inatisha kidogo.

Kwamba marehemu hakuwa na karatasi yoyote?
 
Kwa kuitizama video, Haiwez kuwa congo hapo,
1.uniform za polisi wa zambia
2. plate number kwenye gari ndogo ni ya Zambia pia
3. Wanasikika wakizungumza Bemba (Ligha ya Zambia) na kiswahili chenye lafudhi hiyo pia kwa baadhi ya wazungumzaji.
Nilichofanya ni kujaribu kueleza Mukambo ipo wapi na si uniform, plate number au lugha.

Mokambo is a town on the Congo Pedicle road in the Democratic Republic of the Congo, on the border with Zambia. As of 2012, it had an estimated population of 23,663. Wikipedia
 
Trump hajawahi kusema "shithole country" bali alisema "shithole". Hilo neno country mnaongezaga nyinyi mliopo kwenye hizo shitholes.
 
Apumzike kwa amani...tajiri lazima awe ameshajua....wana track gari zote GPS ya Satelite ...akiona no movement muda wana puga simu kwa driver....au gari zingine.....
 
Askari amekufa kwenye mstari wa majukumu
Rest easy Champ
Wanaume tunaitafuta sana heshima ila wake zetu ni kisanga
MUNGU atusaidie
 
Wamiliki wa malori waache kuwabebesha madereva kemikali zenye sumu za migodini kama loose cargo .Hizo kemikali zinatakiwa zibebwe ndani ya container lililokuwa sealed. Sijui wanakwepa gharama ama vp ? Ila wajue kuwa wanahatarisha maisha ya watanzania maskini. Dereva hawezi kulala gesti kila sehemu anayofikia kutokana na gharama za matumizi pindi awapo barabarani ..na hizo safari za DRC zinaweza kumchukua mtu hadi miezi miwili Go and return. Pesa wanayolipwa haikidhi mahitaji.
 
Back
Top Bottom