Video: Dogo wa miaka 15 ampeleka rafiki yake kwa mganga ili amtoe kafara ya utajiri

Video: Dogo wa miaka 15 ampeleka rafiki yake kwa mganga ili amtoe kafara ya utajiri

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Tena kafara yenyewe sio kama hizi zenu za kiswahili ya kwenda kwa mganga akwambie umtoe ndugu yako kafara ukikubali ndugu yako anaumwa tumbo anakufa la hasha ila ni kafara kama ile ya kumtoa kondoo wa sadaka yani mtolewa kafara anachinjwa damu yake ina mwagwa kwenye madhabahu ya mganga husika " Ritual Killing"

Ilikuwa hivi dogo alienda kwa huyo mganga kumwambia anataka utajiri wa kafara, mganga akamuuliza yupo tayari kumtoa kafara mtu wake wa karibu dogo akasema hilo sio suala kabisa, then mganga akamwambia ni mtu wake yupi wa karibu ambae dogo yupo tayari kumtoa, dogo akajibu rafiki yake wa karibu, basi mganga akwamwambia kesho njoo nae ila ukiwa unakuja nae asijue anakuja kutolewa kafara utajua mwenyewe una mdanganya vipi hadi ufike nae hapa kilingeni.

Bahati nzuri ni kwamba huyo mganga ana hofu ya Mungu na utu ndani yake na hiyo kumwambia dogo amlete rafikiye kwa mganga lengo haswa lilikuwa kumuokoa mtolewa mtarajiwa na pia kumsaidia dogo mtoa kafara kuvungia hiyo mitikasi ya kafara. Mganga akafanya set up akaandaa polisi , waandishi na camera.

Hapo kwenye video Dogo mtoa kafara na mtolewa wapo kilingeni kwa mganga.

Mganga ana muuliza maswali ya kizushi dogo huyu ndio rafiki yako uliye mleta kwa ajili ya kumtoa kafara dogo anajibu ndio. Then anamuuliza upo tayari kumchinja wewe mwenyewe dogo anajibu ndio nipo tayari. Wakati akijibu maswali hayo, dogo mtolewa mtarajiwa anashindwa kuamini anacho kiona kama ni kweli au anaota, akimsihi rafiki yake asimfanyie hivyo na kumwambia mganga kwamba yeye kwao ni mtoto pekee katika familia kwa hiyo wasimuue.

Dogo anaulizwa ukipata pesa yapo utafanya nini, dogo anajibu atanunua Bmw, Royce Locye na kujenga nyumba kali na kuwa na wanawake wengi wazuri.

Thanks God baadae mganga alimuhandle dogo mtoa kafara wannabe kwa vyombo vya usalama ili apate ushauri nasaha kuhusu upuuzi anaotaka kuufanya na dogo mtolewa mtarajiwa ku regain his freedom.


# huyo dogo aliye taka kutolewa ataishi na tatizo labTrust Issue maisha yake yote sidhani kama atakuja kumuamini tena binadamu yoyote maishani..

 
Malezi ya kiimani yako chini sana, na ukichangia na maisha ya mfumo wa kibepari, wachache ndio wanaofaidi.
Sana halafu dogo alikuwa hamuangalii victim wake machoni yani ni kama alikuwa anasema ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni.

Mganga anamwambia sema " money" na yeye anajibu " money"
 
Ukiiangalia video,tumbo la uzazi lazima likuume😥 kijana mtolewa kafara anavyobembeleza
Wazaramo wanasema " sungu la udere linauma mno"

Anyways what I thank God ni kwamba dogo hakutolewa kafara. Ningeumia sana moyoni kama dogo angetolewa kafara.

Moyo wangu ungepata tabu kama moyo wa Yesu alivyo pewa taarifa za kifo cha rafiki yake Lazaro
 
Hiyo sio solution huko maofisini ndio kuna ushirikina hatari mi nadhani tuwafanye madogo wawe na hofu ya Mungu
Nyie ndio hao hao mnawananga kwamba wanakula ugali WA shikamoo halafu ni majobless , greed inachochewa na vitu kama hivi , jamii inawapush watu kuamini material wealth ndio kitu cha muhimu kuliko kila kitu . sasa ngoja wawagawane Kwa kafara , kuna vitu tunaweza kuwa tunavifanya kila siku kwenye jamii kumbe ndio vinacreate downfall yetu kama jamii , twende Tu tutafika
 
Elimu ya dini na makuzi mema ya watoto ndo cha msingi. Kijana huyo angekuw na miak 20 hapo maish yamemgus kdg angetoa ukoo mzima kafar, wazazi mpate la kujifunza hapa.
Kabisa mkuu . 15 years !!! The young boy is so so cold
 
Sometimes huwa namlaumu Mungu kwa kunipa moyo mwepesi na hata mtu akinifanyia ubaya huwa ni rahisi kumsamehe lakini kwa nilichokiona hapo kama ni kweli daah.. Forgive me Lord 🙌🙌
Mi hapo tukitoka tu lazima yeye ndo nimpoteze kiukweli kweli😠
 
Back
Top Bottom