Tuangalie hii video fupi kisha kila mtu atoe yake ya moyoni
View attachment 1860475
Ni clip yenye funzo kwetu wanadamu.
Mwanzoni, anaonekana kijana anaeuza mikanda akijongea meza ya waheshimiwa wanaopata mapochopocho.
Kutokana na hadhi yao, yule muuza mikanda anaonekana msumbufu tu kwao na asiyestahili kuwa pale. Yule baba anamwondoa kwa dhihaka. Ingawa yule mama anaonekana kuwa tofauti na ile tabia ya mwenzie.
Wakati wakiendelea na mlo, ghafla yule baba anakabwa na chakula/kinamkwama.
Kumbe yule kijana anamafunzo juu ya kuokoa mtu aliyekwamwa na chakula na ndiye anakuja kumsaidia.
Baadaye, yule kijana alimpa maelezo yule boss. Kitu ambacho hata yeye aliumia, nadhani yule kijana ana elimu nzuri tu ila hajabahatika kupata kazi.
Funzo:
Moja, tusiwazarau watu kwa mwonekano wao dhidi ya ulionao kwani bado ni hazina kwa upande mwingine.
Mbili, tusilipe kisasi kwa wale waliotutendea ubaya.