Kwa kawaida watu wengi wasio na makazi nchini USA ni wale wa asili ya Afrika, sasa najiuliza, kundi hili tu ndio wavivu wa kufanya kazi? Kundi hili tu ndio wahanga wa madawa ya kulevya? Au ni tatizo la kimfumo zaidi?
Lakini pia, kwenye video hapo chini, kwa siku za hivi karibuni, na wale wa asili za kizungu na asia pia wamekuwa wengi zaidi, au ni uchumi tu umekuwa mgumu? Maana wanakuwa wengi kuliko hawa weusi sasa.
Kwa kawaida watu wengi wasio na makazi nchini USA ni wale wa asili ya Afrika, sasa najiuliza, kundi hili tu ndio wavivu wa kufanya kazi? Kundi hili tu ndio wahanga wa madawa ya kulevya? Au ni tatizo la kimfumo zaidi...
Lifestyle ya huko ni tofauti kabisa na hapa bongolala, ombaomba wa majuu unaweza kuta anamiliki hadi gari ya kutembelea.
Hata nchi za ulaya ambako weusi ni wachache bado utawakuta hao hao weupe kwenye baadhi ya mitaa wanaomba, kwa hiyo siyo kweli kwamba ombaomba weupe hawakuwahi kuwepo, kwamba wameibuka hivi majuzi.