Video: Hebu tujadili kasoro za mkutano wa Tundu Lissu na waandishi wa habari (Sehemu ya KWANZA)

Video: Hebu tujadili kasoro za mkutano wa Tundu Lissu na waandishi wa habari (Sehemu ya KWANZA)

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267

Courtesy: SK Media Online TV

Saga la Tundu Lissu kutangaza nia kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA (T) ili kumrithi mwenyekiti wa sasa Mh. Freeman Mbowe linaendelea kuzua mjadala ndani na nje ya nchi yetu...

Katika video hii, utatazama na kusikiliza uchambuzi murua wa kasoro za mkutano wa Tundu Lissu (Press Conference) aliyoifanya mbele ya wanachama wenzake wa CHADEMA pamoja na waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali vya ndani na vya kimataifa tarehe 13/12/2024 unaofanywa kwa njia ya video na mwandishi wa habari za kiuchunguzi Ndugu Ansbert Ngurumo anayeishi uhamishoni nchini Uingereza....

Tafadhali weka MB kidogo kwenye simu au computer yako kisha tazama video hii mwanzo mwisho...
 
Haya

Ngurumo alikuwa mfanyakazi wa familia ya Mbiwe
Tupo katika dunia huru. Kama ambavyo Tundu Lissu ana uhuru wa kutoa maoni akasikilizwa hivyo basi na akina Ngurumo pia wana haki ya kutoa maoni yao yakasikilizwa bila kujali walikua kina nani kabla.
 
Haya

Ngurumo alikuwa mfanyakazi wa familia ya Mbiwe
Hiyo familia ya Mbiwe iko wapi..?

Au una maana ya familia ya Freeman Mbowe...?

Kama ndiyo hivyo, so what.?

Kwamba, hastahili kusema kuhusu Tundu Lissu au Freeman Mbowe...?
 
Tupo katika dunia huru. Kama ambavyo Tundu Lissu ana uhuru wa kutoa maoni akasikilizwa hivyo basi na akina Ngurumo pia wana haki ya kutoa maoni yao yakasikilizwa bila kujali walikua kina nani kabla.
Hakuna aliyebisha 🐼
 
Hiyo familia ya Mbiwe iko wapi..?

Au una maana ya familia ya Freeman Mbowe...?

Kama ndiyo hivyo, so what.?

Kwamba, hastahili kusema kuhusu Tundu Lissu au Freeman Mbowe...?
Nimetoa Wasifu wake kwamba alikuwa ni Mhariri wa Gazeti la propaganda linalomilikiwa na family ya Mbowe

Very simple 😄
 
Ndio maana hakuna tija kujihusisha na vyama vya siasa. Jihusishe na Rais pekee na Rais atajihusisha na chama chake cha siasa
 
The Palm Beach ,

..waandishi wa habari walimuuliza maswali Lissu kwa uhuru kabisa. Na Lissu aliyajibu bila kukwepa.

..yeyote anayetaka kumfanyia Lissu tathmini ktk hii nia yake ya kuwa mwenyekiti atafaidika akisikiliza maswali na majibu ya siku ya press conference.
 
Back
Top Bottom