- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Askofu Wolfgang Pisa O.F.MCap ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi. Septemba 25, 2025 Askofu Pisa aliongoza Adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha jubilei ya miaka 100 ya seminari kuu ya Mt. Paulo Mtume Kipalapala Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.
Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Askofu Pisa na kuambatanishwa kichwa cha habari kinachosema 'Rais wa TEC awahimiza wakatoliki kushiriki Uchaguzi'
Je, ni upi uhalisia?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia marejeo ya video umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kwa kukata na kuunganisha vipande visivyohusiana hatimaye kutengeneza ujumbe unaopotosha uhalisia.
Akizungumza katika homilia yake kwenye Adhimisho la Misa Takatifu ya kilele cha jubilei ya miaka 100 ya seminari kuu ya Mt. Paulo Mtume Kipalapala Jimbo Kuu Katoliki la Tabora alipiga marufuku kwa watawa wa kike na kiume na kiongozi yeyote wa kanisa katoliki kujihusisha na kampeni za siasa au kutambulishwa na chama chochote cha kisiasa kama mshirika wao.
Aidha aliongeza kuwa haitaruhusiwa kwa mtawa yeyote au mseminari katika mazingira yeyote yale atakayeruhusiwa kujihusisha na jambo lolote lenye taswira ya kisiasa hata kama mtawa angekuwa na ndugu mwenye kujihusisha na siasa.
Vilevile aliwasisitiza kabla ya kwenda kupiga kura tathmini kidogo dhamiri kwani dhamiri inaweza kuwa potofu isipokuwa na uelewa wa kutosha
"Kabla ya kwenda huko tathmini kidogo dhamiri yako, lakini dhamiri inaweza kuwa potofu isipokuwa na uelewa wa kutosha. Tuachane na dhamiri potofu, dhamiri yako itakuwaje safi na kamili? Kwanza muwe na uelewa wa kutosha kwa hicho unachoenda kufanya, Usikilize dhamiri yako kuhusu Ukweli na ile iliyo sawa kwamba katika hili kweli ni lipi? na lililo la haki ni lipi? Soma neno la Mungu likuongoze, Pitia amri za Mungu, Sali juu ya hiyo, ihoji dhamiri yako na hapo ufanye uamuzi wako."