- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Jamii Forums naomba mfanye Check ya hii video kubaini ni ya zamani au ya hivi karibuni. Binafsi niliona hii video kwenye post za wazungu kusoma comments nikaona wanasema video ni ya Zamani sana.
Lakini cha kushangaza video hii inaendelea kutrend na kuaminika ni ya jeshi la wauza madawa wakitishia serikali baada ya El Mencho kuuwawa. Mmoja wapo aliyepost ni Farhan ambaye ni muandishi wa Clouds akihisi ni video ya hivi karibuni
Naomba tupate ukweli
Lakini cha kushangaza video hii inaendelea kutrend na kuaminika ni ya jeshi la wauza madawa wakitishia serikali baada ya El Mencho kuuwawa. Mmoja wapo aliyepost ni Farhan ambaye ni muandishi wa Clouds akihisi ni video ya hivi karibuni
Naomba tupate ukweli
- Tunachokijua
- Kiongozi hatari wa biashara ya dawa za kulevya nchini Mexico, Nemesio Oseguera Cervantes maarufu kwa jina la El Mencho, ameripotiwa kufariki dunia baada ya kujeruhiwa na risasi katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika Jimbo la Jalisco nchini humo.
Madai
Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kikiwainesha wanaonekana kuwa ni wanajeshi wakiwa na vifaa pamoja na magari ya kijeshi na kudaiwa imesambazwa na kundi la Jalisco New Generation Cartel (JNGC) kwa lengo la kuonesha wapo tayari kulipiza kisasi.
Uhalisia wa Taarifa hiyo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa si ya mwaka 2026 kama inavyodaiwa na baadhi ya vyanzo.
Ufuatialiaji kwa kutumia google reverse image search umebaini kuwa video hiyo ilichapishwa mtandaoni kuanzia mwaka 2020 na vyanzo mbalimbali vilichapisha taarifa pamoja na video hiyo.
Mexico daily monitor iliripoti kuwa waziri wa ulinzi wakati huo Luis Cresencio alieleza kuwa video hizo mbili zimetolewa na kikosi maalum cha operesheni cha Jalisco New Generation Cartel