Video inayoonesha gari inayotembea kwenye barabara iliyopo mlimani huku likiwa na mawe mawili juu yake.
Mdau Shiriki kuthibitisha, je, video hii ni halisi au imetengenezwa?
Mdau Shiriki kuthibitisha, je, video hii ni halisi au imetengenezwa?
- Tunachokijua
- Akili mnemba (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.
Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.
Kadri muda unavyokwenda ndivyo ambavyo teknolojia hii inaimarika kutokana na maboresho yanayofanyika kutokana na namna ambavyo watu wanatumia kulingana na mahitaji yao na ndio maana watu wanahofia juu ya siku zijazo kushindwa kutofautisha maudhui halisi na yale yaliyotengenezwa na teknolojia ya akili mnemba kutokana na kuongezeka kwa ufanisi wa utendaji wake mfano mzuri ukiwa ni maudhui ya video, picha na sauti.
Video inayoonesha gari inayotembea ikiwa na mawe juu yake ni halisi au imetengenezwa?
Uhalisia
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa Video hiyo hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili mnemba (AI) Pia kifaa cha utambuzi wa maudhui ya video yaliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia hii kinabainisha kuwa asilimia 99 picha hiyo imetengenezwa kwa Akili Mnemba.
Aidha video hiyo imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanadhihirisha kutengenezwa kwa kutumia akili mnemba. Sehemu ya madhaifu hayo ni pamoja na kuruka kwa maji sehemu ya tairi katika ardhi isiyo na maji, mawe yaliyopo juu ya gari kutokusababisha madhara yoyote kwenye gari hiyo licha kuonekana kuwa makubwa na yenye uzito mathalani nembo ya aina ya gari inapitiwa na jiwe lakini hakuna ukinzani au kuvunjwa, mawe kupotea mara baada ya kudondoka.