- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mwanaume mmoja akiendelea kula chakula wakati watu wengine wakiendelea kujificha kutokana na shambulizi lililotokea kwenye tukio lililotokea Aprili 25, 2025 huko nchini Marekani.
Uhalisia wa tukio hilo
Tukio hilo lilitokea kweli kwa siku hiyo ambapo vyombo mbalimbali pia Ikiwmeo BBC walichapisha taarifa pamoja na video inayomuonesha mwanaume huyo akiendelea kula wakati wenzake wakiwa wanajificha baada ya shambulizi.
BBC walichapisha video halisi pamoja na ujumbe uliokuwa ukisomeka;
“Hakukuwa na uwezekano hata kidogo ningelala chini kwenye sakafu chafu ya Hilton nikiwa nimevaa tuxedo yangu mpya.”
Wengi wa waliohudhuria White House Correspondents' Dinner walijificha chini wakati milio ya risasi iliposikika—lakini kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa tofauti.
Mtu huyo, aliyetambulika kama Michael Glantz, alionekana akiwa ametulia kabisa akiendelea kula saladi yake huku watu waliomzunguka wakikimbilia kujificha kutokana na tukio lililokuwa linaendelea mbele yao."
Uhalisia wa video hiyo
Video iliyowasilishwa na mdau kutaka uhalisia wake, imeharirirwa kwa kutumia teknolojia ya AKili Unde kutoka katika halisi.
Video hiyo inaoonekana kuwa na baadhi ya dosari zinazoonesha kuwa video hiyo ina viasharia vya AI, mathalani mwanaume huyo anaonekana kushika umma na baadae kutokuonekana unapopotelea wapi na matendo mengine yanayokosa uhalisia.
Aidha nyenzo za kidigitali zimebainisha kuwa video hiyo ina viashiria vya kutengenezwa kwa teknolojia ya AI.