Madai
Chapisho la Facebook lililoandikwa kwa lugha ya Hausa liliadai ndege isiyo na rubani ya Iran iliingia kwenye anga la Nigeria na kuangushwa na jeshi la Nigeria katika kijiji cha Dan Isah, jimbo la Sokoto. Chapisho hilo lilijumuisha video ikionyesha mabaki ya ndege hiyo.
“Ndege ya Iran ambayo ilipoteza mwelekeo iliingia Nigeria, na jeshi la Nigeria limefanikiwa kuirushia chini katika kijiji cha Dan Isah, jimbo la Sokoto.”
Uhalisia
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidijitali video halisi
iliyochapishwa mnamo mwezi Machi 1, 2026, na Rudaw Media Network, kituo cha habari cha Kuurd. Video hiyo inaonyesha ndege isiyo na rubani iliyopinduka katika kijiji cha Girdechal, Erbil, katika eneo la Kurdistan, Iraq.
Hakuna ushahidi nchini Nigeria, wala ripoti kutoka vyombo vya habari vya Nigeria au vya kimataifa kuhusu ndege ya Iran nchini Nigeria. Jeshi la Ulinzi la Nigeria halikutoa taarifa yoyote kuhusu kuangusha ndege ya Iran.