POTOSHI Video hii ni ya wananchi wa Venezuela wakishangilia baada ya kukamatwa kwa Rais Maduro

POTOSHI Video hii ni ya wananchi wa Venezuela wakishangilia baada ya kukamatwa kwa Rais Maduro

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwaipaya anasema video hii ni Mamlillion ya Wananchi wa Venezuela wapo mtaani wakishangilia Dicteta Maduro kutolewa madarakani.



Screenshot 2026-01-04 084830.png
 
Tunachokijua
Januari 03, 2026 Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kuwa Marekani ilifanya mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Venezuela na kufanikiwa kumkamata Rais wa nchi hiyo, Nicolás Maduro, pamoja na mke wake.

Kupitia taarifa aliyotoa kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema operesheni hiyo ilifanywa kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya Marekani.

Inaelezwa kuwa tangu Nicolás Maduro achukue hatamu za uongozi mwaka 2013, Venezuela imepitia misukosuko mikubwa ya kisiasa na kijamii ambayo imesababisha shutuma nzito za ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiandika ripoti mbalimbali zinazoonyesha mbinu za kimfumo zinazotumiwa na Serikali kudhibiti upinzani na kukandamiza uhuru wa raia.


Video inayosambazwa mtandaoni

Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoniikionesha umati mkubwa wa watu nakudaiwa kuwa ni Wananchi wa Venezuela walioingia mtaani kushangilia baada ya Rais Maduro kutolewa madarakani.

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliajiuliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa video hiyo haihusiani na tukio la kukamatwa kwa Rais Maduro kwani si ya Januari 2026 bali iliwahi kuchapishwa mtandaoni Julai 30, 2024 ambapo mwandishi wa habari wa Mexico LupitaJuarez alieleza kuwa ni maandamano yaliyoendelea nchini Venezuela kufuatia matokeo yaliyomtangaza Nicolás Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais.

Kadhalika ukurasa wa Alerta Mundial kwenye mtandao wa X ulichapisha video hiyo na kuandika "Mitaa ya Venezuela imefurika kwa waandamanaji wakipinga udanganyifu wa uchaguzi unaodaiwa kufanywa na Nicolás Maduro."

​
screenshot-2026-01-04-085118-png.3524980
​
Back
Top Bottom