KWELI Video hii ya gari kugonga gari nyingine imetengenezwa kwa akili unde

KWELI Video hii ya gari kugonga gari nyingine imetengenezwa kwa akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Vipi mdau! Shiriki kuthibitisha video hii kwa kubainisha dosari unazoziona. Je,Je, zinaakisi uhalisia?


1761401588426.png
 
Tunachokijua

Akili Unde (AI) ni seti ya teknolojia zinazoiwezesha kompyuta kutekeleza majukumu mbalimbali ya kina na kwa uwezo mkubwa kadri ya maelekezo ya mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuona, kuelewa na kutafsiri lugha inayozungumzwa na maandishi, kuchanganua data, kutengeneza picha na video na kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo mbalimbali.

Aidha teknolojia hii imekuwa muhimu katika kurahisisha ufanisi wa shughuli za kila siku na hii ni pindi tu inapotumika kwa nia iliyo njema, lakini inapotumiwa kwa nia ovu huweza kusababisha madhara makubwa kwa watu, mathalani uwepo wa taarifa potofu unachangiwa pia na teknolojia hii ambayo watu hutumia kutengeneza na kusambaza taarifa zisizo sahihi mfano picha, sauti, na video.

Katika kujenga uwezo wa kumuwezesha kila mmoja kutambua maudhui yaliyotengenezwa kwa teknolojia hiyo Wadau wa JamiiCheck kupitia Jukwaa la JamiiCheck.com na mitandao mingine ya kijamii wameshiriki kuthibitisha video inayoonesha gari ndogo ya abiria ikigonga gari aina ya Range Rover, ambapo wengi wao wakisema imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde huku wakibainisha dosari zinazokinzana na uhalisia.

Mfano Brown_Mwangosi Mdau wa JamiiCheck Instagram amebainisha kuwa "Hiace ina watu wawili lakini ukiangalia kwa makini baada ya kutoka hao watu wawili nafasi ya dereva anajitokeza mtu from no where, Range iliyogongwa sehemu ilipogongwa inajirudi na kuwa kama haijagongwa, lundo la watu wanaokimbia haieleweki wametokea wapi"

Vilevile Cuthbert S. Mpangala mdau wa JamiiCheck Facebook anabainisha dosari mbili ambazo ni "1. Gari zote hazijaonesha uhalisia wa kuharibika baada ya ajari. 2. Abiri wanaonekana wakitoka mbele ya Gari na sio mlangoni"

Kadhalika JamiiCheck kupitia nyenzo za kidijitali imejiridhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa akili unde. Pia uwepo wa mapungufu yasiyo ya kawaida yanadhihirisha kutumika kwa teknolojia ya akili unde kutengeneza video hiyo, mathalani gari iliyogongwa kujinyoosha yenyewe pasipo jitihada zozote za kiufundi, namba kubwa ya watu wanaotoka sehemu isiyokuwa na mlango kwenye gari ndogo ya abiria.
​
screenshot-2025-10-28-080138-png.3494935

screenshot-2025-10-28-080214-png.3494936

screenshot-2025-10-28-080234-png.3494937
Gari limegongwa alafu hapo hapo linajitengeneza upya... Kuna abiria kama vile kashukia kupitia kioo cha mbele wakati halijavunjika...


Cc: Mahondaw
 
Hao abiria wameshukia vipi upande wa Julia?
 
Back
Top Bottom