SI KWELI Video hii ya gari yenye mzigo ikidondoka ni halisi?

SI KWELI Video hii ya gari yenye mzigo ikidondoka ni halisi?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.

1775473986198.png
 
Tunachokijua
Wadau wa JamiiCheck kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii wameshiriki kubainisha uhalisia wa video inayoonesha gari likiwa limebeba magodoro na mtu akiwa juu yake iwapo ni halisi au lah!

Ambapo wengi wameshiriki kwa kubainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa video hiyo kutokuwa halisi kutokana na baadhi ya dosari zinazoonekana, mathalani baadhi waliandika;

Kivuli hakihusishi kivuli cha mzigo uliopo juu ya gari, pia mzigo haukuwa umefungwa na chochote, hivyo usingeweza kusogea hata hatua moja bila kudondoka.
Ni kwamba waliegesha juu ya gari bila kufunga kamba?. AI asante.
Hata iwaje yule mtu wa juu tu asingeweza kuwepo hapo kama kweli.

JamiiCheck imefuatilia kwa kutumia nyenzo za kidigitali na kujiridhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kutumia AI
1775724577842-png.3569869
Back
Top Bottom