KWELI Video hii ya huyu Twiga si halisi, imetengenezwa kwa AI

KWELI Video hii ya huyu Twiga si halisi, imetengenezwa kwa AI

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Video ni hii, wakuu


1771591764649.png
 
Tunachokijua
Wadau wa JamiiCheck wameshiriki kuthibitisha uhalisia wa kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonesha Twiga akidondoka kutoka katika gari baada ya kujigonga katika daraja.

Wengi wamebainisha kuwa video hiyo ina viashiria vinayoonesha kuwa video hiyo si halisi. Miongoni mwa sababu zilizotajwa ni uzito wa Twiga haundeni na namna alivyodondoka, lakini pia mnyama huyo baada ya kudondoka alionekana kuwa na miguu miwili badala ya mitatu.

Uhalisia wa video hiyo ni upi?

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hiko cha video kimetengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde (AI).

Licha ya dosari zinazoonekana kama zilivyobainishwa na wadau lakini pia kupitia nyenzo za kidigitali za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde JamiiCheck imebaini kuwa video hiyo imetengenezwa ama kuhaririwa kwa AI.
1771846919024-png.3547602
Ufuatiliaji wa video hii unaonyesha kuwa video hii si ya kweli na imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kompyuta (CGI/VFX) ambayo inafanya kazi kama Akili Unde

Katika kufuatilia zaidi inaonesha, mwili wa twiga unapoanguka barabarani hauna uzito wa asili. Twiga ni mnyama mkubwa na mzito, lakini hapa anaonekana kama mdoli wa plastiki anapogonga lami na kuruka-ruka kidogo (bounce) bila kuleta athari yoyote kwa gari wala barabara.

Tukio hilo ambalo linasambaa sana mtandaoni imetengeza video kwa kurejelea tukio la nyuma ambalo linaelezea tukio la kweli lilitokea nchini Afrika kusini 1/08/2014 Ambapo wanyama walikuwa wakisafirishwa kuelekea bustani ya wanyama iliyoko Warmbarths, kama Kilomita 160 yaani maili 99 nje ya Johannesburg.

walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini Johannesburg.

Katika tukio hilo shuhuda moja Thinus Botha aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa alikuwa akiendesha nyuma ya Lori hilo akashuhudia namna Twiga huyo alivyojigonga kwenye Daraja la Garsfontein barabara ya N1 ya Johannesburg' huku twiga hao wakitokwa na Damu nyingi

Wanyama wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama, lakini shirika la kutetea haki za wanyama la NSPCA lilisema twiga mmoja alikufa.
 
Back
Top Bottom