KWELI Video hii ya Mamba kukimbizwa na binadamu imetengenezwa kwa AI

KWELI Video hii ya Mamba kukimbizwa na binadamu imetengenezwa kwa AI

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Wakuu, hii uhalisia wake ni upi?
1770793024142.png

 
Tunachokijua
Kupitia mtandao wa X mtumiaji mmoja alichapisha video inayomouonesha mamba akifukuzwa na binadamu katika bwawa iliyoambatana na ujumbe kuwa Mamba hakutegemea hili.

Wadau wa JamiiCheck wameshiriki kuthibitisha uhalisia wa video hiyo iwapo ni halisi ama si halisi. Ambapo wemgi wamebainisha kuwa video hiyo si halisi kutokana na baadhi ya dosari zinazoonekana.

Mathalani walieleza kuwa sauti ya maji yanayosikika haiendani na tukio husika, aidha tukio la mamba kukimbizwa na binadamu si la kawaida. Dalton elijah aliandika;

Licha ya hivyo mamba ni wanyama wanaohitaji mazingira maalum ya ikolojia. Uwepo wa mamba kwenye dimbwi dogo sana la maji, kama inavyoonekana kwenye video, hauendani na tabia za asili za mnyama huyo. Hali hii inatia shaka uhalali wa tukio hilo.

Uhalisia wa Video hiyo

JamiiCheck imefuatilia kipande hicho cha video na kujirirdhisha kuwa video hiyo imetengenezwa kwa tekbolojia ya Akili Unde (AI).

Video hiyo ina matendo yasiyo ya kawaida mathalani kiwango cha maji kwenye dimbwi hilo hayawezi kumfanya mtu huyo kuzama kama inavyoonekana.

Aidha kwa kutumia nyenzo za kidigitali za kubaini maudhui yaliyotengenezwa kwa Teknolojia ya Akili Unde umebainisha kuwa video hiyo si halisi.
1771139793378-png.3544223
Huko mbele ya safari kumkamata mwenzio ana chiti ni itabidi iwe "USO kKWA MACHO" vinginevyo atasingizia AI

Weka video mkuu, tuione ndio tutoe neno
 
Kwa kutumia nyenzo ya Ai video detector inabainisha kuwa video hii mjengeo imetengenezwa na akili unde kwa sababu ya binadamu anaibukia kwenye dimbwi la maji huku mamba akionekana kukimbia kwenye vichaka kwa kasi na namna isiyoendana na uhalisia wa kimaumbile

Licha ya hivyo mamba ni wanyama wanaohitaji mazingira maalum ya ikolojia. Uwepo wa mamba kwenye dimbwi dogo sana la maji, kama inavyoonekana kwenye video, hauendani na tabia za asili za mnyama huyo. Hali hii inatia shaka uhalali wa tukio hilo.
 
Back
Top Bottom