Kupitia mtandao wa X mtumiaji mmoja alichapisha video inayomouonesha mamba akifukuzwa na binadamu katika bwawa iliyoambatana na ujumbe kuwa Mamba hakutegemea hili.
Wadau wa JamiiCheck wameshiriki kuthibitisha uhalisia wa video hiyo iwapo ni halisi ama si halisi. Ambapo wemgi wamebainisha kuwa video hiyo si halisi kutokana na baadhi ya dosari zinazoonekana.
Mathalani walieleza kuwa sauti ya maji yanayosikika haiendani na tukio husika, aidha tukio la mamba kukimbizwa na binadamu si la kawaida. Dalton elijah aliandika;
Licha ya hivyo mamba ni wanyama wanaohitaji mazingira maalum ya ikolojia. Uwepo wa mamba kwenye dimbwi dogo sana la maji, kama inavyoonekana kwenye video, hauendani na tabia za asili za mnyama huyo. Hali hii inatia shaka uhalali wa tukio hilo.
Kwa kutumia nyenzo ya Ai video detector inabainisha kuwa video hii mjengeo imetengenezwa na akili unde kwa sababu ya binadamu anaibukia kwenye dimbwi la maji huku mamba akionekana kukimbia kwenye vichaka kwa kasi na namna isiyoendana na uhalisia wa kimaumbile