- Source #1
- View Source #1
Soko la Afrika lililo kati ya Kongo na Gabon ambapo wazazi maskini walileta watoto wao kuuza, kwa vile hawawezi kuwalisha. Afrika iko kwenye matatizo makubwa
NB: Nimeiweka hii mada huku kwa ajili ya kutafuta uhalisia wake!
NB: Nimeiweka hii mada huku kwa ajili ya kutafuta uhalisia wake!
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na Taarifa inayosambaa ikiambatana na video ikielezwa kuwa ni ya soko la watumwa ambapo wazazi wanauza watoto wao.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa taarifa hiyo imekuwepo mtandaoni angalau miaka miwili iliyopita na si ya mwaka 2026 kama ambavyo imesambaa tena. Mathalani tazama hapa.
Vyanzo vya awali vilivyochapisha taarifa hiyo vimeeleza kuwa hali hiyo ilitoka katika mpaka wa Congo na Gaboni ambapo wazazi wanafanya kitendo hicho kutokana na ugumu wa maisha. Chanzo kimoja kilichapisha video hiyo Noveba 25, 2023 kiliandika;
"Hapa ni mpakani mwa Congo na Gabon, kutokana na ugumu wa maisha wazazi wanalazimika kuwauza watoto wao kwa wanaohitaji ili kupata pesa ya kuendeshea maisha."
Tovuti ya reliefweb iliachapisha makala yake mwaka 2012 na kueleza kuwa kumekuwa na ongezeko la watoto kusafririshwa kutoka katika mataifa yao kwenye kwenye mataifa yenye utajiri wa mafuta. Nchi hizo zilizotajwa ni Gaboni, Equatorial Guinea and the Republic of Congo.