Kuna video inayosambaa kwa kasi kwenye mtandao wa TikTok na majukwaa mengine, ikidai kuonesha dakika za mwisho za msemaji wa kundi la M23, Willy Ngoma, akishambuliwa na kuuawa na ndege zisizo na rubani (drones). Video hiyo inahusishwa na mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na jeshi la serikali ya DRC (FARDC) katika eneo la Rubaya, Kivu Kaskazini.
- Tunachokijua
- Kuna video inayosambaa kwa kasi kwenye mtandao wa TikTok na majukwaa mengine, ikidai kuonesha dakika za mwisho za msemaji wa kundi la M23, Willy Ngoma, akishambuliwa na kuuawa na ndege zisizo na rubani (drones).
Video hiyo inahusishwa na mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na jeshi la serikali ya DRC (FARDC) katika eneo la Rubaya, Kivu Kaskazini.
Uhalisia wa video hiyo ni upi?
Ufuatiliaji umejirirdhisha kuwa video hiyo si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya AKili Unde. Video hiyo ina mapungufu ya mwenendo usio wa asili.
Kwa kutumia nyenzo za kubaini maudhui ya yaliyotengenezw kwa AI mfano nyenzo ya Hive ya Moderation inabainisha kuwa Video hiyo imetengenezwa kwa AI kwa asilimia 97.3.
Tukio hili limetengezwa kwa kurejelea tukio la kweli ambapo Msemaji huyo aliuawa kupitia shambulio la angani lililotekelezwa na FARDC eneo la Rubaya Jumanne usiku, shambulio ambalo liliwaacha viongozi kadhaa wa M23 na majeruhi.