View attachment 1653914
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kuwa ni aggressive na mkali, lakini hatujawahi kumwona akishika kiboko kucharaza viboko watu hadharani...!!
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kwamba hapendi wahalifu na matumizi mabaya ya rasrimali za nchi ikiwemo fedha, lakini hajawahi kuamuru wahujumu uchumi, watakatishaji fedha ama wezi wa mali ya umma wapigwe risasi ama viboko hadharani....
Rais John Pombe Magufuli, huponda na kufokafoka kwa maneno makali na ya kuudhi (sometimes) lakini huamuru uchunguzi kufanyika na hatua za kawaida za kikazi na kisheria kutendeka...
Huyu DC yeye ni nani hasa hata afanye ujinga kama huu? Kwa kweli simuelewi na sijui kama nitamwelewa...!
View attachment 1653943
HAPA JAMAA ANATENDA UJINGA, ANATOA HUKUMU...
Polisi wangekuwa na mtazamo na akili kama za huyu DC, basi mpaka sasa kusingekuwa watu magerezani maana wangekuwa wanahukumiwa papo hapo kwenye tukio...
Jamii hususani watoto wajifunze nini toka kwa kiongozi kama DC huyu anayejitetea kwa ujinga wa matendo yake?....
Je, jamii ijifunze na kuona kuwa kumbe ni sawa watu kujichukulia sheria mkononi kwa wanaowadhania ni "wahalifu" ama "wakosaji" kama alivyofanya DC?..
Kama mtazamo wa DC ndivyo ulivyo, kumbe basi, hakuna haja ya kuwa na mahakama Tanzania..
Baada ya kuona uhalifu huo, kila mtu angetarajia kumuona DC akiamuru watu hao anaodhani ni wahalifu wakipelekwa mahakamani, lakini looh, DC akadhani yuko juu ya sheria na kujiamulia mwenyewe adhabu ya kuwapa....!
Sijui ni kwanini huyu DC mpaka sasa bado yuko ofisini maana amekosa sifa za kuwa kiongozi ktk nafasi hiyo asilani...!!