Ndio yale yale ya siku zote, Watanzania hupelekeshwa kwa mpigo mmoja. Kitu kama hiki hauwezi kukiona huku Kenya maana hamna sheria ya kuzuia muda wa mabasi kusafiri. Kwa Bongo huwa inabidi mabasi ya mikoani yatoke yote muda wa masaa ya asubuhi ili yasafiri mchana wote na kufika mida ya saa mbili hadi saa nne usiku, la sivyo yanalazimishwa kuegeshwa pembeni abiria wanalala njiani.
Kuna mshikaji wangu juzi amesafiri kwenda Iringa tokea Dar, ilibidi basi liegeshwe walale njiani, sheria za ajabu hizo.
Niliwahi kusafiri kwenda Arusha, tulitoka Dar kama tumechelewa mida ya saa saba, iltulazimu kulala Moshi, ilinibidi kukodi chumba maana upumbavu wa kulala kwenye basi siwezi.
Kwa Kenya, usafiri wa usiku ni ruksa, hivyo hamna haya mahangaiko ya kusongamana, mabasi yanaondoka muda wowote.