I wish u would come up with statistical report tht point out tht Kenyans are the most victim kwnye issue kama hzo.....ningekuelewa vzur..........unless unaleta ur personal claims for all Kenyans
You can't get such statistics because most go unreported, hivi utakwenda kuwasema wapi, yaani kwa mfano uhangaishwe na polisi halafu uende kwenye kituo cha polisi kuwasema?
Binafsi nafahamu matukio kadhaa ambayo Wakenya wamewahi kupitia magumu huko. Kuna Mkenya mmoja kwenye bar alikua anakunywa pombe yake na kucheza muziki hana issue na mtu, halafu pembeni kuna maafisa wa uhamiaji ambao walikua wanapata beer zao, baadaye wakabaini jamaa ni Mkenya kwa lafudhi yake.
Wakamkamata na kuanza kumhoji, yeye alikua na stakabadhi zake, lakini jamaa kwa jinsi walikua walevi hawakutaka kumskliza, wakajitoa ufahamu na kuondoka naye usiku, baadaye wakarudi naye kwenye bar na kumuamrisha awaagizie beer kwa muda wote watakua hapo.
Mwengine alikua anatokea kula usiku akakumbana na mapolisi kwenye defender, wakaanza kumhoji, walipogundua ni Mkenya, yaani hawakutaka hata kuangalia vyeti vyake, walimkamata na kuondoka naye na kuzunguka usiku wote akiwa kwenye defender hadi mida ya saa tisa usiku wakamuachia aende zake. Jamaa alifika nyumbani ila asubuhi akakwenda kituoni na kuomba aongee na mkuu wao, akamhadithia masaibu yake ya usiku na kumuonyesha mkuu vyeti vyake halali ambavyo mapolisi hawakutaka hata kuvisoma, mkuu akampa pole tu na kuahidi atachunguza, yakaishia hapo.
Visa vipo vingi tu, binafsi sijakumbana navyo, lakini nawafahamu Wakenya wengi tu ambao walishayapitia, kunaye ambaye polisi walimnyang'anya simu bila hata aibu. Mara nyingi huwa nawaambia Watanzania ambao hawaamini, siku moja wajaribu kuendesha gari lenye namba za usajiri za Kenya, safiri nalo tokea Namanga hadi Dar halafu uniletee mrejesho.