SI KWELI Video ikimuonesha Mbappe akicheza mpira na Roboti

SI KWELI Video ikimuonesha Mbappe akicheza mpira na Roboti

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Salaam Wakuu,

Nimekutana na Video ikimuonesha mchezaji wa PSG Kylian Mbappe akicheza mpira na Roboti. Kuna ukweli kuhusu video hii?

Tunaombeni ufafanuzi.

1703698580093.png



Video iliyosambaa mtandaoni
 
Tunachokijua
Kylian Mbappé ni mchezaji wa mpira wa miguu (Raia wa Ufaransa) anayekipiga kunako Klabu ya Paris Saint Germain (PSG). Mbappe amezaliwa mjini Paris na kukulia Bondy, Mbappé alianza kukipiga rasmi katika klabu ya Monaco mwaka 2015, ambapo alishinda ubingwa wa Ligue 1 msimu wa 2016–17.

Mwaka 2017, akiwa na umri wa miaka 18, Mbappé alijiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa kudumu wenye thamani ya €180 milioni, hivyo kumfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi na mchezaji kijana ghali zaidi wa wakati wote. Zaidi ya hayo, Mbappe ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa.

Tangu August 27, 2023 kupitia Mitandao ya Kijamii Instagram na X kumezuka video yenye takriban sekunde nane ikimuonesha mchezaji Mbappe akiwa anashindana kupiga faulo na Roboti. Video hiyo inaonesha Roboti akifunga goli kisha kufurahia huku mchezaji Kylian Mbappe akionekana kushangazwa na uwezo wa Roboti huyo.

Upi ukweli kuhusu Video hii?
JamiiCheck imefatilia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa video hiyo haina ukweli bali imetengenezwa kwa kuhariri video ya mtu halisi kuingiza picha ya Roboti.

Mathalani, akaunti ya rasmi ya YouTube ya Boom imeichambua video hii na kubaini kuwa video inayosambaa ikimuhusisha Mbappe na Roboti sio halisi bali imetengenezwa. Boom wanaeleza kuwa katika video halisi Mbappe alikuwa akicheza mpira na Ousama Nacer mtengeneza maudhui wa YouTube ambapo picha yake imehaririwa na kumfanya afanane na Roboti.

JamiiCheck pia imepitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Ousama Nacer na kubaini kuwa video hiyo akiwa anacheza mpira na Mbappe aliiweka katika ukurasa wake tangu Desemba 23, 2022.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo, JamiiCheck imejiridhisha kuwa video inayosambaa ikimuonesha Roboti na Mbappe wakicheza mpira ni ya kutengenezwa.
Back
Top Bottom