SI KWELI Video ikimuonesha mwanaume akiwa mtupu akikimbia baada ya kukutwa na mke wa mtu

SI KWELI Video ikimuonesha mwanaume akiwa mtupu akikimbia baada ya kukutwa na mke wa mtu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna video inasambaa twiter na Instagram ikimuonesha mwanaume akiruka dirisha na kukimbia huku akiwa mtu kabisa bila nguo, watu hao wamekuwa wakishare video hiyo na kuweka ujumbe wa MKE WA MTU SUMU wakimaanisha mtu huyo alikuwa na mke wa mtu kisha akafumaniwa ndio anakimbia.

Je, ni kweli mtu huyo anakimbia fumanizi na tukio hilo limetokea Tanzania?

JamiiCheck, msaada wa kujua ukweli.

1717194188876.png



 
Tunachokijua
Kumekuwa na video inayosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikimuonesha mwanaume mmoja ambaye anakimbia kabla ya kugongwa na gari, mwanaume huyo anaonekana kuwa hana nguo jambo ambalo limekuwa likihusishwa na fumamizi na baadhi ya watu kwenye mitandao wakidai tukio hilo na kuwa mtu huyo alikutwa akiwa na mke wa mtu.

Je, ukweli ni upi?
Tukio hilo la mwanaume kukimbia mtupu lilitokea nchini Marekani katika jimbo la California jijini Los Angles(LA) ambapo video inaonyesha wakati mwanamume aliyekuwa uchi huko California alipogongwa na gari baada baada a kujaribu kuukwepa msongamano mkubwa wa magari na kisha kujikuta akigongwa na kupaa juu ya sehemu ya mbele ya gari kudondoka chini.

Video hiyo, ambayo imesambaa kwa kasi, inamuonyesha mwanamume huyo aliye uchi akiruka uzio kwenye nyumba ya familia yake na kukimbilia barabarani. Anafaulu kukwepa gari moja lakini kisha anakutana na gari jingine linalomgonga.
agongwa-na-gari-jpg.3004301
Taarifa zinaeleza mwanaume huyo alikuwa akisumbuliwa na afya ya akili kabla ya kuruka ukuta wa nyumbani kwao na kukimbia, inaelezwa familia yake walikuwa wamewapigia simu polisi kutokana na changamoto hio kabla mtu huyo kukimbia.
1717121154607-png.3004302
Baadaye polisi walifika na kumpeleka hospitali kupatiwa matibabu.

Jamiicheck imebaini kuwa taarifa zinazodai mwanaume huyo alikimbia baada ya kukutwa na mke wa mtu ni taarifa za uzushi, mwanaume huyo alikutwa na tukio hilo kutokana na changamoto ya afya ya akili na si fumanizi.
Back
Top Bottom