POTOSHI Video ikiwaonesha Ulaya wakishangilia goli la Yanga dhidi ya Simba

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu huko mtandaoni nimekutana na hii video imenipa utata, je ni kweli hawa wazungu walikuwa wanashangilia goli la yanga dhidi ya simba? Msaada tafadhali katika kupata uhalisia wa video hii wakuu




Your browser is not able to display this video.

 
Tunachokijua
Simba na Yanga ni timu za soka ambazo zilianzishwa miaka ya 1935 na 1936 zikiwa na ushindani wa kisoka huku zikiwa na mchango mkubwa wa kuitangaza Tanzania kupitia mashindano ya kimataifa lakini pia zikitumika kuwakutanisha wapenzi wa mpira wa miguu pamoja wakijulikana kama watani wa jadi.

Mechi yoyote inayowakutanisha vigogo hawa kutoka mitaa ya Kariakoo jijini Dar es salaam huwavutia watu wengi kwani umekuwa ukifuatiliwa na wapenzi wa soka ndani ya Tanzania, Afrika na hata nje ya Afrika.

Mnamo tarehe 19 mwezi Oktoba 2024, ilichezwa mechi ya watani hao wa jadi kati ya Simba na Yanga ukiwa ni muendelezo wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2024/2025 mzunguko wa kwanza ambapo, Yanga waliibuka na ushindi mwembamba wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Simba.

Mara baada ya mchezo huo kumekuwapo na video inayosambaa mtandaoni inayoonesha watu (wazungu) wanaofuatilia mchezo huo kwa njia ya televisheni wakishagilia goli walilolipata Yanga mara baada ya Simba kujifunga na kudaiwa kuwa ni mashabiki wa Yanga kutoka nchini Uingereza.

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Reverse Image Search umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kwani haihusiani kabisa na mchezo kati ya Simba na Yanga uliochezwa Oktoba 19, 2024.

JamiiCheck imebaini kuwa video halisi ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika mtandao wa YouTube mnamo tarehe 16 Juni 2016 wakati wa mashindano ya mataifa ya Ulaya (EURO) na video hiyo ikonesha mashabiki wakifuatilia mchezo kati ya England dhidi ya Wales kupitia televisheni kubwa iliyopo katika uwanja wa Ashton Gate stadium uliopo katika jiji la Bristol nchini Uingereza.

Tumebaini video inayopotoshwa kuwa ni mashabiki wa Yanga kutoka Uingereza wakishangilia mara baada ya timu hiyo kupata goli, inaonesha televisheni ikichezacheza pembeni tofauti na video halisi ambayo televisheni inayotazamwa video yake ikiwa imetulia, hii inaonesha uthibitisho wa kuhaririwa kwa video hiyo.

Mashabiki hao walikua wakishangilia goli lilofungwa na Daniel Sturridge dakika ya 91 na kuifanya England kuibuka na ushindi wa mabao 2 - 1 dhidi ya Wales.

Aidha video ambayo inayoonesha mashabiki hao wakishangilia huku televisheni ikionesha goli la Yanga dhidi ya Simba imehaririwa kutoka kwenye uhalisia wake kwa kuondoa picha ya video halisi na kuweka picha ya video ya mchezo kati ya Simba na Yanga katika televisheni hiyo.

Kadhalika juni 16, 2016 kituo cha Televisheni cha CBS SPORTS kiliichapisha video hiyo katika tovuti yake kikielezea namna ambavyo mashabiki hao wakishangilia goli la ushindi wa England dhidi ya Wales lilopatikana dakika za mwishoni ikiwa ni moja kati ya mchezo uliochezwa wakati wa mashindano ya Euro 2016.

Video hiyo imehifadhiwa hapa.
Hahahaaaa aiseee sikubaliani na editing za kijinga...Yanga timu kubwa sana haihitaji kiki za namna hiyo.
 
Kweli huko nyuma mwiko wenye akili ni wawilk tu...
Umeshindwa kutambua kuwa hiyo video ghushi.
 
Wanasimba mmechimba mpaka madesa kuprove..furaha ya wanayanga!!!
Ni upumbavu kueneza uongoambao una athari kwa vizazi vya sasa na baadae, kama una tabia hiyo acha. Tabia kama hizi hupelekea hata watu kuzushiana mambo ya hovyo mitandaoni, mfano vifo n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…