- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na video kadhaa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook na Instagram, zikionyesha mamba wakitembea mitaani baada ya kutokea kwa mafuriko nchini Australia.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na video kadhaa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook na Instagram, zikionyesha mamba wakitembea mitaani baada ya kutokea kwa mafuriko nchini Australia.
Hata hivyo, katika ufuatiliaji wa kina imebainika kuwa video hizo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili unde, zikirejelea tukio la kweli lililotokea baada ya mafuriko nchini humo siku ya Jumamosi.
Tukio la kuonekana kwa mamba baada ya mafuriko liliripotiwa katika maeneo ya kaskazini mwa Australia. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa nchi hiyo, wananchi walionywa kuhusu uwepo wa mamba katika maeneo mbalimbali.
Jimbo hilo pia lilipitia mvua kubwa mwishoni mwa juma, huku mji wa Katherine ukikumbwa na mafuriko mabaya zaidi tangu mwaka 1998.
Katika taarifa yao, jeshi la polisi lilinukuliwa likisema:“Kuna mamba kila mahali. Tafadhali usiingie majini. Ujumbe uko wazi kabisa,” walisema.