POTOSHI Video inamuonesha raia wa China akitembea juu ya maji

POTOSHI Video inamuonesha raia wa China akitembea juu ya maji

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
​
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na video inayosambazwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania na katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikimuonyesha mtu anayedaiwa kuwa raia wa China akitembea juu ya maji.

Video hiyo imeambatana na madai kwamba China imegundua au kutengeneza viatu maalumu vinavyomwezesha binadamu kutembea juu ya uso wa maji bila kuzama. Madai hayo yamezua mjadala mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku baadhi wakiamini kuwa teknolojia hiyo ni halisi.

Hata hivyo, uchunguzi wa kidijitali umebaini kuwa video hiyo si ya kweli. Dalili mbalimbali zilizobainika katika video hiyo zinaonyesha kuwa imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde au mbinu nyingine za uhariri wa picha na video.

Katika uchambuzi wa video hiyo, kuna viashiria vinavyoonyesha kutokuwepo kwa mwingiliano wa kawaida kati ya mwili wa mtu huyo na maji. Pia, mwendo wake unaonekana kuwa wa kiajabu na usioendana na kanuni za kawaida za fizikia.​

1780725710675-png.3602071

Aidha, hakuna ushahidi wa kisayansi au taarifa kutoka kwa taasisi za utafiti, kampuni za teknolojia au mamlaka za China zinazothibitisha kuwepo kwa viatu vinavyomwezesha mtu kutembea juu ya maji kwa namna inavyoonekana kwenye video hiyo.

Wabunifu mbalimbali duniani wamewahi kusajili gunduzi za viatu vya kutembea juu ya maji, lakini miundo hiyo huhitaji mifumo maalumu ya kusukuma mwili mbele, kama vile propela ndogo, ili kumsaidia mtumiaji kubaki juu ya maji badala ya kutegemea usawa wa mwili pekee.

Aidha ukurasa wa Wildxroar uliochapisha video hiyo katika Ukurasa wa Instagram Juni 03, 2026 unabainisha kuwa video si halisi bali imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde ambapo umeambatanisha maelezo yanayosema:

"Kila kitu unachokiona hapa kimetengenezwa na akili bandia (AI).

Kinachovutia zaidi ni jinsi akili zetu zinavyokubali haraka kuwa vitu hivi ni halisi. AI imefikia kiwango cha kuweza kuunda wanyama, mandhari na hata dunia nzima zinazoonekana kama za kweli kabisa, hivyo kufanya mpaka kati ya uhalisia na ubunifu wa kidijitali kuwa mgumu kutambua.

Tunashuhudia mabadiliko makubwa ya kiteknolojia ambayo hayajawahi kutokea hapo awali. Siku zijazo hazitakuwa tena kuhusu mashine kuwasaidia binadamu pekee, bali pia kuhusu mashine kuunda vitu vinavyoweza kufanana kwa kiwango kikubwa na uhalisia.

Kadiri AI inavyoendelea kukua, kutofautisha kati ya kilicho halisi na kilichotengenezwa kidijitali huenda kukawa moja ya changamoto kubwa zaidi za zama hizi za kisasa."
​

Attachments

  • CHINA.jpg
    CHINA.jpg
    127.6 KB · Views: 76
Back
Top Bottom