- Source #1
- View Source #1
Wakuu naomba kufahamu uhalisia wa hii video nimeona ikipostiwa mtandaoni kuwa ni wezi wanachomwa huko Arusha
- Tunachokijua
- Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kikiwaonesha watu waishambuliwa na wananchi kwa moto wakiwa na pikipiki, huku ikiwa imeambatana na ujumbe unaoeleza kuwa wanaofanyiwa kitendo hiko ni wezi kutoka Arusha.
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kimtandao na kubaini kuwa ni kweli tukio hilo lilitokea Arusha, kipande cha video kinachosambaa kimekuwepo mtandaoni tangu mwezi wa 07/2024 na imeendelea kuisambaza mara kwa mara kutokea hapo.
Tumebaini tukio hilo lilitokea tarehe 11/07/2024 huko Kaloleni Arusha kwa mujibu wa East Africa Tv (EATV) wanaelezwa kuwa watu hao walituhumiwa kwa kosa la wizi (ukwapuaji) wa simu kwa raia huku wao wakiwa kwenye pikipiki.
Tv ya mtandaoni ya Kusaga (Kusaga Tv) wanabainisha kuwa baada ya washutumiwa hao kufanya tukio hilo muda mfupi baadaye walikamatwa na wananchi wenye hasira kali waliowashambulia na kisha pikipiki waliyokuwa wanaitumia ikachomwa. Shambulizi hilo lilipelekea mmoja wa watuhumiwa hao kupoteza maisha palepale huku mwingine akiokolewa baada ya gari ya polisi kufika.