Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, ameonyesha moyo wa huruma kwa kusaidia mtoto mdogo kumtwisha dumu la maji kichwani baada ya kumkuta akichota maji.
Tukio hilo lilitokea wakati Bashungwa alipokuwa katika pita pita zake, ambapo alikutana na watoto wakichota maji. Akiwa anawaongelesha kwa lugha yao, alijitolea kumsaidia mmoja wao kwa kumtwisha dumu hilo kichwani.
Inaelekea wewe huwa huna desturi ya kusaidia watu nguvukazi maana ni kawaida kwa Watz wengi kusaidiana hasa mtu anapotaka kujitwisha kitu kizito na hata maji ukipita kisimani wamama wanakuomba au wewe mwenyewe unajiongeza (hii hazihusiani na kusaidia hela ila kumtwisha mtu mzigo kawaida)
Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, ameonyesha moyo wa huruma kwa kusaidia mtoto mdogo kumtwisha dumu la maji kichwani baada ya kumkuta akichota maji.
Tukio hilo lilitokea wakati Bashungwa alipokuwa katika pita pita zake, ambapo alikutana na watoto wakichota maji. Akiwa anawaongelesha kwa lugha yao, alijitolea kumsaidia mmoja wao kwa kumtwisha dumu hilo kichwani.
Kwa hiyo umeona hiyo ya maana? Na kesho atakuja kumtwisha? Hiyo imeonyesha ilivyo shida ya maji na yeye anawasaidiaje wapigakura wake.
Kuna kitu amemuuliza kwa kirugha, kwamba anasoma na mtoto akamjibu, hasomi.
Kwa point hizo mbili tu imeonyesha shida ya elimu na maji. Kwa hali hiyo atakuwa hajui shida za watu wake. Hapo hajaongolea afya, hali barabara nk. Mnapoweka video kama hizi fikiria tafsri ya wasomaji!
Kwa maoni yangu: Alitakiwa abebe yeye ili kumsaidia na si kumbebesha mzigo.
Hii inaleta taswira kuwa viongozi wengi kazi yao ni kubebesha raia mizigo wao wakifikiri hayawahusu.